MUSO NDAKI YA DAR WANOLEWA, WAASWA KUZINGATIA SHERIA ZA MZUMBE NA SERIKALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 11, 2022

MUSO NDAKI YA DAR WANOLEWA, WAASWA KUZINGATIA SHERIA ZA MZUMBE NA SERIKALI


Picha ya Pamoja.

Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe,  Dtk. Andrew Sule akizungumza wakati wa Mafunzo ya Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe,  Dtk. Andrew Sule akizungumza wakati wa Mafunzo ya Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi chuoni hapo jijini Dar es Salaam.Naibu Mshauri wa wanafunzi, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam, Zitta Mnyanyi akizungumza wakati wa Mafunzo ya Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi chuoni hapo.Naibu Mshauri wa wanafunzi, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam, Zitta Mnyanyi akiwatunuku vyeti Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya Utawala bora.

VIONGOZI wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam (MUSO)wanolewa kuwa viongozi wazuri wa sasa na baadae.

Naibu Mshauri wa wanafunzi, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam, Zitta Mnyanyi Akizungumza wakati wa Mafunzo ya Utawala mafunzo yaliyofanyika Chuoni hapo mwishoni mwa wiki amewahamasishaViongozi wa MUSO kulizingatia wanayofundishwa na wasifurahie tuu uongozi lakini wafurahiye kutekeleza majukumu yao kwa taratibu na kwanuni walizopewa katika mafunzo hayo ya utawala bora.

Amesema kuwa Julai 9, 2022 wanatoa mafunzo kwa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO) ikiwa ni mwezi miwili na siku 11 zipite tangu wachaguliwe kuongoza wanafunzi wenginge chuoni hapo May  25, 2022

"Lengo kubwa la mafunzo haya ni kuwawezesha wanafunzi waweze kuendesha majukumu yao kwenye serikali ya wanafunzi, lakini pia kuungana na Utawala Chuo Kikuu Mzumbe kuongoza kwa hali ya weredi." Amesema Zitta

Amesema kuwa wamekuwa na taratibu za kutoa mafunzo ya uongozi bora pale tuu wanapochaguliwa viongozi wapya. Na kuhakikisha kuwapa ujuzi Maalumu unaohusiana na Uongozi na utendaji kazi huku wakiendelea na masomo.

"Tunawapa Mafunzo juu ya masuala ya fedha pamoja na bajeti, pia namna ya kuhitisha vikao, kufanya vikao, Kukaimu nafasi mbalimbali na taratibu zake.

"Pia masuala ya mawasiliano na maadili kwa ujumla lakini pia ujuzi kuhusiana na ubora wa kazi na Kushirikiana katika kutatua migogoro na mbinu za utatuaji matatizo mbalimbali yaliyopo kati yao wenyewe na wanafunzi wenzao. Waweze pia kufanya kazi pamoja na zaidi kwa utawala wa serikali ya Chuo Kikuu Mzumbe." Amesema Zitta

Amesema kuwa matamanio makubwa Viongozi wa MUSO kuwa Viongozi wakubwa leo hii wapo Chuoni kama Viongozi wa Serikali ya wanafunzi huenda kesho watakuwa katika ngazi za juu za uongozi wa serikali Mbinu hizo walizopewa zitawasaidia sasa na baadae.


"Mafunzo wanayopewa nina uhakika wakianza kuyafanyia kazi katika uongozi wao yatawasaidia kuwa kwenye kumbu kumbu zao kuwa walitekeleza majukumu Chuo Kikuu Mzumbe wataweza kutekeleza majukumu yao makubwa ambayo yatakuwa mbele yao kwaajili ya Jamii na kwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Amesema Zitta

Amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe Kinakanuni na taratizbu zake ambazo zinafanya utawala kutoa mafunzo hayo ili wasiende kinyume na mfumo wa Chuo hicho pamoja na Mfumo wa Kitaifa.

Kwa Upande wa Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam(MUSO), Zauda Halisi amesema kuwa Mafunzo hayo yanawawezesha ukujua namna ya kuongoza wanafunzi wenzao pamoja na jamii kwa ujumla kwa pale watakapo maliza masomo yao.

"Katika hii semina tumejifunza mambo mbalimbali kuhuuana na Uongozi sisi kama viongozi wa serikali ya Wanafunzi tunatakiwa tuongoze Vipi, tuisheje katika kukamilisha malengo yetu na malengo ya Chuo chetu."

"Tunaimani kabisa tukitoka hapa tutakuwa na ufahamu Mzuri ambao utatusaidia baadae kuwa viongozi wazuri wa kuongoza taifa." Amesema Zauda

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia katika maisha ya baadae kwa sasa ni viongozi wa wanafunzi lakini katika malengo ya baadae na ndoto za kutumikia Serikali. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad