HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2022

KAMPUNI YA TIGO, ISUZU WAKUDISHIANA MAGARI 45


Meneja Mawasiliano wa wa Kampuni Tigo Tanzania, Woinde Shisael  katika akikata utepe kuashiria makabidhiano ya magari 45 leo Juni 28,2022.

KAMPUNI ya Specialized Rentals Limited (SRL) ni inayotoa huduma bora ukodishaji wa uendeshaji wa vifaa vya moto hapa nchini imekodisha Kampuni ya TIGO Tanzania (MIC TPLC) magari aina ya Pickups 45.

Akizungumza leo Juni 28, 2022 jijini Dar es Salaam leo Meneja Mkuu wa Kampuni ya Specialized Rentals Limited, Mihir Patwardhan amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa magari bora zaidi na yenye kiwango cha juu pia ikiwa na vifaa vya kufavyia matengenezo pindi yanapokuwa na hitilafu ili kumrahisishia mtumiaji wa magari hayo.

“Hivi karibuni Specialized Rentals Limited imepewa oda ya Ugavi wa Pickups 45 Mpya aina ya ISUZU D-MAX na kampuni ya TIGO Tanzania ambapo wanaendeleza falsafa yake ya kutoa huduma bora kwa mteja.”

“Tunajisikia furaha kubwa kuchaguliwa na Tigo Tanzania kwa utaratibu huu adhimu. Shukrani zetu za dhati kwa Bw. Anurup Chatterjee na timu yake kwa kuweka imani katika huduma zetu bora tunazozitoa. Tuna uhakika wa kutumia uzoefu wetu tulionao ili kuhakikisha ufanisi unapatikana na unakuza biashara zetu na shughuli zetu zinazofanyika kwenye makampuni yetu kukidhi mahitaji ya wateja wetu".  Amesema Patwardhan

Ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuweka mkazo katika kujenga miundombinu ya barabara zenye viwango vya kimataifa nchini kote, hivyo kuwezesha na kuvutia uwekezaji nchini na miundombinu hii bora imekuwa ikichochea uwekezaji wa ndani na wa nje ya Nchi.

Akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Innocent Rwetabura, Meneja Mawasiliano wa wa Kampuni hiyo, Woinde Shisael amesema kuwa ushirikiano wao ni wa kimkakati na Specialized Rentals Limited ambao wanaungwa mkono na kampuni maarufu ya Al Mansour (Isuzu) kwa kuipa kampuni ya Tigo ili kuweza kutoa huduma zake nchi nzima kwa kuwa wana magari yenye uhakika na ufanisi zaidi.

Kwa Upande wa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Al Mansour – Isuzu amesema ‘Al Mansour’, Anurup Chatterjee, amesema kuwa mfanyabiashara aliyeidhinishwa wa ISUZU amewekeza dola milioni 1.5 katika soko la Tanzania tangu kuanzishwa kwake na uwekezaji huo umeonyesha imani kwa Kampuni ya ISUZU katika sekta ya vifaa vya moto hususani magari na masoko katika uchumi wa kikanda.

“Kwa miaka mingi tumeonyesha juhudi katika kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa usafiri hasa usafiri wa kutumia magari na tumehakikisha tunatoa huduma bora za usafiri nchini ikiwa ni sehemu ya msaada wake katika kuhakikisha huduma za usafiri zinakuwa bora na nafuu nchini.” Amesema Chatterjee

Aina za magari ya Isuzu yameunganishwa mahususi na kurekebishwa kuendana na hali ngumu ya kimiundombinu ya Afrika Mashariki. Aidha, Isuzu imeweka mtandao imara baada ya mauzo ili kusaidia wateja wake katika sekta binafsi na ya umma ili kuhakikisha magari yao yanaendelea kutumika katika eneo lolote lile na kwa vipengele hivyo wanatarajia kuleta matokeo chanya kwa wateja wa Tigo Tanzania na wateja wa Kampuni hiyo hapa nchini.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Specialized Rentals Limited, Mihir Patwardhan akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2022 wakati wa kukubalina na Tigo kukodisha Magari 45. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa wa Kampuni Tigo Tanzania, Woinde Shisael.
Meneja Mawasiliano wa wa Kampuni Tigo Tanzania, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2022 wakati wa kukubalina na Tigo kukodisha Magari 45, Kulia ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Specialized Rentals Limited, Mihir Patwardhan na kushoto ni Mkuu wa Kampuni ya Al Mansour – Isuzu amesema ‘Al Mansour’, Anurup Chatterjee.

Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Ndeshi Rajabu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2022 wakati wa kukubalina na Tigo kukodisha Magari 45 wengine kutok kushoto ni Mkuu wa Kampuni ya Al Mansour – Isuzu amesema ‘Al Mansour’, Anurup Chatterjee, Meneja Mawasiliano wa wa Kampuni Tigo Tanzania, Woinde Shisael na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Specialized Rentals Limited, Mihir Patwardhan.
Meneja Mawasiliano wa wa Kampuni Tigo Tanzania, Woinde Shisael akikata keki wakati wa Makabidhiano ya Magari 45 leo  June 28, 2022 jijini Dar es Salaam.
Wanyakazi wa Kampuni ya Specialized Rentals Limited (SRL) wakikabidhi Mfano wa Funguo kwaajili ya kukabidhiana magari 45 na wafanyakazi wa Tigo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad