ACCO yahimiza matumizi salama ya Internet - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 30, 2022

ACCO yahimiza matumizi salama ya Internet

 


*Fursa za Kazi,  Ufadhili , Mikopo ya Fedha katika Mitandao zimewafanya wengi kutapeliwa

Na Mwandishi Wetu 

Muungano ya Mashirika ya Matumizi ya kukabiliana na janga la Uhalifu wa Mitandao (ACCO) limesema kuwa  katika ukuaji wa matumizi ya Internet kumekuwa na matumizi yasio salama na kufanya baadhi ya watu kutapeliwa kwa njia ya mitandao hivyo kunahitaji nguvu ya pamoja katika kutumia matumizi salama.

Akizungumza na Waandishi wa habari wa Habari Mratibu wa ACCO Shuubert Mwarabu  amesema kuwa taarifa za Interpol na Afripol ya Novemba 2021 ilionesha ongezeko kubwa la uhalifu wa mitandao wa Internet Barani Afrika kutokana na idadi kubwa ya vijana.

Amesema kuwa mwaka 2020 takribani asilimia 60 ya watu Barani Afrika ilikuwa na  watu wa wenye umri chini ya  miaka 25 hivyo kwa kipindi kifupi imeongezeka na uhalifu wa mitandao umeongezeka ambapo jitihada lazima zifanyike katika utoaji wa elimu ya matumizi hayo.

Mwarabu amesema wakati wa  ugonjwa  wa UVIKO 19 dunia iliwekeza nguvu kukabiliana na igonjwa huo ambapo baadhi ya watu wakatumia wa mitandao  kutokana na sekta nyingi kuathiriwa kutokana watu kutumia mbinu tofauti za kujipatia kipato hata kama ni kinyume cha sheria na taratibu.

Amesema kwa Tanzania kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Aprili 2021 Tanzania ilikadriwa kuwa na watumiaji wa mtandao wa Internet takribani ya milioni 21 ambapo idadi yake inaendelea kukua.

Mwarabu amesema katika uhalifu wa mitandao wanaofanyiwa ni makundi yote bila kujali elimu ambapo wenye elimu ndio wanafanyiwa utapeli zaidi.

Aidha amesema janga lingine katika matumizi ya internet inakwenda katika usafirishaji haramu wa binadamu ambapo wasichana wanakumbwa kwa kuingia urafiki wa mahusiano kwa njia ya mtandao na mwisho wa siku msichana anaondoka nchini na kwenda kwa mtu na kufanyisha biashara ya ngono.

Hata hivyo amesema kuwa kumekuwepo kwa matukio ya ulaghai katika mitandao ikiwemo udanganyifu katika Kazi, Mapenzi, Mikopo , Fursa za Masomo, Ufadhili pamoja na  Uwekezaji.

Amesema ACCO inaamini kuwa kasi ya maendeleo ya kidijitali ni lazima iendane na kasi ya  elimu juu ya usalama mtandao kwa kuanzisha program za elimu kwa jamii.

 Amesema watu waache kukuparika na fursa zinazopatikakana katika mitandao bila kwanza kujiridhisha na kudhibitisha kuwa fursa hizo ni za kweli.


Mratibu wa Muungano wa Mashirika ya Kukabiliana na Uhalifu wa Mitandao ya Internet (ACCO) Shubert Mwarabu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utapeli katika mitandao jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji Ramadhan Kilasi akizungumza kuhusiana na kutumia sanaa yake katika kufikisha elimu sahihi ya kutumia mitandao , jijini Dar es Salaam
Mtangazaji Flora Enock akizungumza namna wasichana wanavyotapeliwa katika mitandao kuhusiana na mahusiano , jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad