HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 1, 2022

Taasisi ya Ustawi yaendelea kugusa makundi maalum na Jamii inayozungka kampasi zake

 Wananfunzi wa Shule ya msingi Mangara wakiwa katika utulivu wakisikiliza kwa makini waliokuwa wakifundishwa na wahadhiri na wataalamu wa ustawi wa jamii kutoka Taasisi ya Ustawi wa jamii Kisangara na kijitonyama Dar es Salaam. 

Picha ya Pamoja; walio keti, kutoka kulia Rufina Khumbe mhadhiri msaidizi ISW, Mkuu wa kampasi ya ISW Kisangara Dkt. Minani Ntahosanzwe, Mwl. wa nidhamu David Mcharo shule ya msingi Mangara, Dunstan Haule mhadhiri msaidizi na mhadhiri msaidizi ISW Kisangara Gladness Mnisi, Pamoja na wanafunzi wa Shule ya msingi Mangar na wanataaluma wa ustawi wa jamii kutoka kampasi ya Kisangara.
 Mwanataaluma wa Ustawi wa Jamii Zena Mwena kutoka ISW kampasi ya Kisangara akizungumza na wanafunzi wa darasa la nne mpaka la saba wa shule ya msingi Mangara ambapo Taasisi ya Ustawi wa Jamii walifika kutoa elimu.
Picha Na Ofisi ya Uhusiano -ISW

Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro
WAHADHIRI wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Dar es Salaam na kampasi ya Kisangara mwishoni mwa juma wametembelea shule ya msingi Mangara iliyopo Kisangara Mwanga, mkoani Kilimanjaro kwa dhumuni la kutoa elimu na kuongea na wanafunzi wa shule hiyo kuhusiana na masuala ya ukatili, viashiria vyake, haki zao za msingi, na namna ya kuripoti vitendo hivyo katika mamlaka husika, vile vile nidhamu na maendeleo ya kielimu.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliyochini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, ukiacha kazi yake kuu ya kutoa elimu ya kitaaluma ya Ustawi wa Jamii, pia ina jukumu la kuifikia jamii na kutoa elimu na msaada wa kisaikolojia kwa jamii yetu.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Mkuu wa Kampasi ya Taasisi ya Ustawi wa jamii Kisangara Dkt. Minani Ntahosanzwe amesema kupitia mpango wa taasisi wa ushiriki jamii katika kuleta afua kwa changamoto mbali mbali katika jamii kampasi hiyo inakutana sio tu na watoto (wanafunzi) bali jamii kwa ujumla kuhusu masuala ya familia, uchumi, na maendeleo

“mfano ni vikundi vya akina mama (Vikoba) ambavyo vipo katika mpango wetu na tunawatembelea na kuzungumza nao ni namna gani wanasonga mbele katika mipango yao ya kimaendeleo kiuchumi, halikadhalika kuwajengea uwezo kutambua masuala ya Ukatili na kuyaripoti sehemu husika’’.

Naye mwalimu wa nidhamu wa Shule ya Msingi Mangara Mwl. David Mcharo akiongea kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema vitendo vya ukatili vipo katika jamii ya vijiji wanapotoka wanafunzi wa shule hiyo, mfano, ni watoto kuadhibiwa kwa kupigwa kiwango cha ukatili na wazazi wao wenyewe, watoto kutumikishwa kufanya kazi ambazo sio zao, kwa mfano kuchunga na shughuli nyingine za mtaani ambazo hazina tija na kusababisha watoto kukosa shule na hali ya utoro kuwa juu.

“Wazazi wengi hawajui haki, wajibu na mahitaji ya watoto na ndio maana unakuta watoto wanazaliwa mijini lakini nawaletwa kwa bibi na babu kulelewa, na malezi ya bibi na babu yanakuwa hahfifu, uwezo wa bibi na babu kutoa chakula na mahitaji ya kielimu kama madaftari, sare za shule, kalamu na chakula ni mdgo au haupo na kwa uji huu wa walimu kutoka ustawi wa jamii watoto hawa wamepata kitu kipya na watoto wamefunguka zaidi kimawazo na kuelewa kumbe kuna sehemu ya kusemea matatizo yetu na kuna watu wa kuyasikiliza na kuyatatua. Alisema Mwl. David mcharo.

Kwa upande mwingine mhadhiri msaidizi Zabibu Mbangwa kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kisangara amesema kwa sasa kampasi hiyo sasa itaweza kuendelea na kazi za kutoa elimu na shughuli za ushirikishaji jamii katika kutoa elimu ya masuala mbali mbali kwa jamii inayotuzunguka baada ya kuongezewa ujuzi na uzoefu kutoka kwa wahadhiri wa kampasi ya kijitonyama Dar es Salaam ambao wamekuwa hapa katika kampasi yetu ya Kisangara kwa siku mbili pamoja na wanafunzi wetu hapa kampasi ya kisangara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad