HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2022

MAFANIKIO MAKUBWA BANDARI YA MTWARA…!

Meli ya MV. EGT Southern Cross ikiendelea kupakia shehena ya Makaa ya Mawe yanayotarajiwa kusafirisha kwenda Amsterdam Uholanzi. 

Meli ya MV. EGT Southern Cross ikiendelea kupakia shehena ya Makaa ya Mawe yanayotarajiwa kusafirisha kwenda Amsterdam Uholanzi. Meli hiyo inatarajiwa kupakia Tani 59960 za makaa hayo kwenda Barani Ulaya.
Baadhi ya magari yakipakia shehena ya makaa ya mawe kwenda katika Meli ya MV. EGT Southern Cross yatakayosafirishwa kwenda Amsterdam Uholanzi, hii ikiwa ni shehena kubwa zaidi ya Makaa ya Mawe kusafirishwa Kupitia Bandari ya Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti (mwenye kofia) akiwa na viongozi waandamizi wa TPA katika eneo la kupakia Shehena ya Makaa ya Mawe ya Bandari ya Mtwara kushuhudia zoezi la kupakia tani 69960 za Makaa hayo kwenda Barani Ulaya.
Baadhi ya magari yakipakia shehena ya makaa ya mawe kwenda katika Meli ya MV. EGT Southern Cross yatakayosafirishwa kwenda Amsterdam Uholanzi, hii ikiwa ni shehena kubwa zaidi ya Makaa ya Mawe kusafirishwa Kupitia Bandari ya Mtwara.

MELI ya MV. EGT Southern Cross inatarajia kusafirisha Tani 59960 za Makaa ya Mawe kwenda Amsterdam Uholanzi, hii ikiwa ni shehena kubwa zaidi ya Makaa ya Mawe kusafirishwa Kupitia Bandari ya Mtwara.

Akizungumza leo mjini hapa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Bw. Nicodemus Mushi amesema, usafirishaji wa Shehena hii kubwa kwenda Bara Ulaya ni hatua muhimu ya kulifikia Soko kubwa la Bara la Ulaya baada ya bidhaa hiyo kuwa na Soko la uhakika katika Bara Asia.

Akifafanua zaidi alisema shehena kubwa ya mwisho ilikuwa tani 59815. "Hii ndio Mara ya kwanza kwa shehena kutoka Bandari ya Mtwara kwenda Bara la Ulaya moja kwa moja," alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa Masoko na Uhusiano, Bw. Mushi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza alisema, Serikali ya Mkoa wa Mtwara inaridhishwa na utendaji wa TPA na Bandari ya Mtwara hasa katika kutafuta wateja.

Alisema uwekezaji wa Serikali mkoani Mtwara ni mkubwa, ikiwemo Ujenzi wa gati ambao umegharimu Shilingi Bilioni 157.8.

Aidha aliongeza kuwa Serikali imeiwezesha TPA kununua vitendea kazi na kuboresha mazingira ya kufanya kazi hivyo kuna kila sababu ya kuunga mkono jitihada hizi za TPA.

"...Ili kupata Wateja zaidi na sasa Mwelekeo Uwe katika Nchi Jirani ya Comoro ambayo ina fursa kubwa ya kufanya Biashara na Tanzania. Kwa kushirikiana na Kampuni ya Ruvuma Coal tunaendelea kutafuta Masoko zaidi ili kuufanya uwekezaji wa Serikali katika Bandari ya Mtwara kuwa na tija," alisema Brigedia Jenerali Gaguti. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad