HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 22, 2022

WATANZANIA TEMBELEENI HIFADHI YA PUGU-KAZIMZUMBWI INA VIVUTIO VYA KUPENDEZA NA KIHISTORIA-NDANDIKA

Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
March 21

IDADI ya watalii wanaotembelea Msitu wa Hifadhi ya Pugu-Kazimzumbwi, wilayani Kisarawe ,mkoani Pwani imeongezeka ndani ya kipindi cha miaka miwili kutoka watalii 533 hadi kufikia 13,000 .

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kutokea Mkoani Pwani, waliokwenda kutembelea vivutio hivyo ,mhifadhi wa misitu  kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Kisarawe Fred Ndandika alisema ,zaidi ya asilimia 70 ni watalii wa ndani na waliobaki ni watalii toka nje ya Tanzania.

Alisema kuwa idadi hiyo inaongezeka kutokana na kuitangaza na uboreshaji wa miundombinu ya utalii ambayo iko jirani na Jiji la Dar es Salaam.

"Msitu huu wa Hifadhi una mazingira asilia na tunatoa huduma ya utalii ikolojia ambapo kuna vivutio vingi ndani ya Msitu na utalii ulianza mwaka 2016/2017."

Alieleza kuna vivutio vingi, ikiwemo kupanda mlima wenye km .2 kupanda na kushuka km.2,Bwawa la Minaki wanatoa huduma ya michezo ya uvuvi ,kupiga Kasia na kuongeza vibanda vya kupumzikia wageni , pia wanaendelea kuboresha barabara ,ili kufungua barabara ya km .10 Pugu -Kazimzumbwi kwa kiwango cha Changalawe ili kufungua fursa zaidi.

Akitoa maelezo ya vivutio mbalimbali kwa watalii wa ndani ,Omary Sharif alisema, Kitengo Cha maliasili na utalii kulikuwa hakuna kitengo Cha udhibiti kwahiyo udhibiti wake haukuwa mzuri Lakini Sasa Kuna Wakala wa Misitu( TFS ambao wanashughulika na Misitu, kufanya doria na kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka msitu juu ya mimea na athari zake na kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.
Pia kuna chemchem inayotiririsha maji Hadi katika bwawa , kutokea katika pango la mzimu wa MAVOGA anaetokana na kabila la kizaramo.

"Huyu mzimu ana taswira aina mbili ya Joka kubwa na nyingine ni mzungu mwenye kitumbo wazi kavaa kipensi,kitumbo wazi ,na hii taswira ya joka kubwa sio Kama ananionyesha tuu ukimuona jua kuna kitu hakipo sawa , katika pango lake kuna tanda siafu hiyo inakuwa mmoja hayupo sawa kulingana na masharti yake."alifafanua Sharif.

Vilevile Sharif alieleza, katika hifadhi hiyo utakuta mti wa Mpugupugu ambao Ni mmea maarufu pamoja na mmea Tiba mwingine unaojulikana Kama mnaki haupatikani sehemu nyingine Duniani zaidi ya kupatikana kwenye hifadhi hiyo ,kwa kuenzi jina hilo ndipo shule ya Sekondari Minaki ilipopatiwa jina hilo ili jina lisipotee .
"Hutojutia kuja kutembelea hifadhi hii, Nawaomba wananchi wajenge tabia ya kutoka kujionea vivutio vilivyopo ndani ya nchi Yao ,kimoja wapo Ni hiki Cha Kazimzumbwi "aliongeza Sharif.

Mtalii wa ndani, Malietha Kileo -mkazi wa Dar es Salaam alisema ,wengi wamezoea kuona vivutio vya milima Kilimanjaro na hifadhi huko Arusha ,Mikumi ,Ngorongoro Lakini wananchi wanapaswa kujua kuna hifadhi asilia Kazimzumbwi ambayo ni nzuri inavutia.

Waandishi wa habari kutoka Mkoani Pwani,waliojumuika na waandishi wa habari wengine kutembelea hifadhi hiyo, John Gagarini na Gustavo Haule walisema wamefurahi ,wameweza kupanda mlima, haikuwa rahisi kwani ni umbali wa masaa matatu-manne kupanda na kushuka .
 "Kupanda mlima ni zoezi tosha,tujenge tabia ya kufanya mazoezi ili kujenga afya zetu, Sisi tumekuja kutembelea hifadhi lakini tumepanda na mlima, niwaombe wananchi wenzangu waje kutembelea vivutio hivi". alieleza Gagarini.

Alisema,utalii unasaidia kujiliwaza,kujua utalii uliopo nchini ambapo katika sehemu hiyo Serikali inanufaika na Pato linalotokana na utalii wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad