HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 23, 2021

NEC YATOA ELIMU YA MPIGA KURA JIMBO LA NGORONGORO

Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakitoa vipeperu kwa wananchi wa kata ya Nainokanoka kijiji cha Mainokanoka kitongoji cha Emunge leo kwenye jimbo la Ngorongoro mkoa wa Arusha. TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na zoezi la utoaji wa Elimu ya mpiga kura kwa njia ya ana kwa ana kwa wakazi wa jimbo la Ngorongoro ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Mbunge jimbo la Ngorongoro.


Elimu hiyo inatolewa kwa kutembelea kaya, maeneo ya mikusanyiko. Lengo ni kuwezesha wapiga kura wa jimbo la Ngorongoro kupata taarifa sahihi na elimu kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi ili waweza kuwa katika nafasi nzuri ya kushiriki michakato ya uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kutoa Elimu ya Mpiga kura nchi nzima na kuratibu taasisi na asasi ambazo zinatakiwa kutoa Elimu hiyo kupitia kifungu ha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343.
Elimu ya mpiga kura imetolewa kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Sale iliyopo kata ya Sale , jimbo la Ngorongoro.


Maafisa wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakitoa elimu ya mpiga kura katika tarafa ya Ngorongoro, kata ya Nainokanoka kijiji cha Mainokanoka kitongoji cha Emunge leo kwenye jimbo la Ngorongoro mkoa wa Arusha.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad