HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 27, 2021

RAS TABORA AWATAKA WATAALAM WA RHMT NA CHMT KUSOGEZA CHANJO YA UVIKO 19 KARIBU NA WANANCHI

 


NA TIGANYA VINCENT

TIMU ya Afya ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri za Wilaya (CHMT) Mkoani Tabora zimetakiwa kutumia mikusanyiko mbalimbali kutoa elimu na baadaye  chanjo ya UVIKO 19 ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kutoa elimu kwa Wataalamu wa RHMT na CHMT kuhusu Kampeni ya Chanjo ya UVIKO 19 kupitia Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO 19.

Alisema wananchi wengi wako tayari kuchanjwa lakini wakati mwingine umbali wa vituo vya kutolea huduma ndio umesababisha washindwe na kuwa kikwazo kwao.

“Sogezeni huduma hizo katika mikusanyiko kama vile masoko minada  na kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo na kisha ambao watakuwa tayari wachanjwe” alisisitiza.

Alisema chanjo ya UVIKO 19 inagharimu fedha nyingi na hivyo ni vema ikatumika kabla kuisha muda wake wa matumizi.

Makungu alisema Mtaalamu wa Sekta ya Afya ambao chanjo zitamalizika matumizi yake bila kufikishwa kwa wananchi hatakuwa na maelezo ya kujitetea badala yake itakuwa ameonyesha udhaifu wake wa kusimamia masuala mapana ya umma.

Katika nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora aliwataka wataalamu hao kushirikiana na wadau wengine kama vile wanasiasa  wazee maarufu , wakuu wa Wilaya Wakurugenzi Watendaji na watu maarufu  katika kutoa na kupeleka ujumbe sahihi kwa jamii kuhusu umuhimu wao kuchanja.

Alisema ni vema wananchi waelimishwe kuhusu chanjo hiyo inavyosaidia kupunguza hatari ya mtu kufa na matumizi ya kuwekewa miira ya kupumulia.

Aidha Makungu alisema Siku ya Wazee duniani ambayo uadhimishwa tarehe moja Oktoba ,Mkoa wa Tabora utatoa elimu na huduma ya chanjo kwa wazee katika maeneo mbalimbali.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora (RMO) Dkt. Honoratha Rutatinisibwa alisema lengo la mafunzo hayo kwa RHMT na CHMT ni kuwajengea uwezo ili waweze kwenda kufundisha watoa huduma kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma za afya wawe na uelewa wa ugonjwa wa UVIKO 19 na waweze kutoa chanjo kwa wananchi wengi.

Alisema katika kuhikikisha wanasogea huduma kwa wananchi wengi wameongeza Vituo vya Kutoa Chanjo ya UVIKO 19 kutoka 24 hadi kufikia 268 kwa Mkoa wa mzima.

Dkt. Honoratha aliongeza sanjari na hilo pia wataendelea kutoa chanjo ya UVIKO 19 kupitia Huduma za Mkoba kwenye maeneo mabayo yatakuwa hayana Vituo vya Kutolea chanjo kama vile kwenye Minada Masokoni Vyuoni na maeneo yote yenye mkusanyiko.

Aidha Mganga Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwapongeza Mkuu wa Wilaya ya Tabora Sikonge na Uyui kwa kushirikiana na CHMT zao katika kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo hiyo na hivyo kuanza kuongeza idadi ya  ya watu wanaochanja.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akifungua leo mafunzo ya siku mbili ya kutoa elimu kwa Wataalamu wa Timu ya Afya ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri za Wilaya (CHMT) kuhusu Kampeni ya Chanjo ya UVIKO 19 kupitia Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO 19.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora (RMO) Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akitoa maelezo leo ya lengo la mafunzo ya siku mbili ya Wataalamu wa Timu ya Afya ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri za Wilaya (CHMT) kuhusu Kampeni ya Chanjo ya UVIKO 19 kupitia Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO 19
Baadhi ya washiriki kutoka Timu ya Afya ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri za Wilaya (CHMT) wakiwa katika mafunzo ya siku mbili ya namna ya kuendesha  Kampeni ya Chanjo ya UVIKO 19 kupitia Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO 19.
Timu wa Waganga Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Tabora wakiwa katika picha ya pamoja leo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (katikati) baada ya kufungua leo mafunzo ya siku mbili ya kutoa elimu kwa Wataalamu wa Timu ya Afya ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri za Wilaya (CHMT) kuhusu Kampeni ya Chanjo ya UVIKO 19 kupitia Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO 19.
Picha na Tiganya Vincent

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad