HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 2, 2021

NIT, LHRC, TCDC WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KUEKAMILISHA MRADI WA EASTRIP

 

Mkuu wa Chuo cha Taifa Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha TCDC, Sara Teri wakionesha Mkataba uliosainiwa leo kati ya NIT na TCDC.
Mkuu wa Chuo cha Taifa Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akiwa na Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu Ana Henga wakionesha mkataba uliosainiwa leo kati ya NIT na kituo cha haki za binadamu (LHRC) jijini Dar es Salaam.

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimesaini  Mikataba wa miwili ya makubaliano kati yake,  Kituo cha Haki za binadamu (LHRC) na Kituo cha Mafunzo, Maendeleo na Ushirikiano (TCDC) leo Agosti 2, 2021 jijini Dar es Salaam.

 Mikataba hiyo inalengo la kuboresha utendaji wa chuo hicho hususani wakati huu ambao chuo kinatekeleza mradi wao wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP)unaofadhiriwa na Benki ya Dunia.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano  hayo leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA), Hamza  Johari  amesema,  ushirikiano huo  utazidi kukiboresha chuo hicho na kukiwezesha kutimiza malengo yake katika kuzalisha wahitimu bora.

"Mkataba huu utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitano unaotekelezwa na NIT wakishirikiana na wadau mbalimbali utakuwa na mambo mengi yaliyowekwa katika utekelezaji wake kiwemo kuwepo na kituo mahili katika kuzalisha wataalamu wanaohusika na nyanja mbalimbali za uzalishaji" amesema Johari.

Makubaliano mengine ni pamoja na  mkataba wa kushughulikia masuala ya uongozi na changamoto za kijinsia iliyosainiwa baina ya Chuo hicho na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) pamoja na taasisi inayojishughulisha na utoaji wa elimu katika masuala ya uongozi ya TCDC.

Amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo kutakaisadia NIT katika mpango wake wa kuzalisha wataalamu wenye umahiri katika sekta ya anga na hatua itakayofanikisha kufikiwa kwa  malengo mengi nm ikiwemo uchumi wa kati.

"Lakini mradi huu ili uweze kwenda vizuri inapaswa kuanzishwa kwa kamati ya ushauri ya mradi itakayokuwa na wajumbe mbalimbali kulingana na weledi wao ambao kazi yao kubwa itakuwa kusimamia utekelezaji wa mradi huu amesema Johari

Amesema moja ya agenda ya Bodi ya wataalam wa Anga wa Dunia ni pamoja na kuwepo kwa vituo vya umahiri katika mataifa mbalimbali jambo ambalo kwa Tanzania linatekelezwa na Chuo NIT.

Amesema kuwa kamati hiyo imeishaanza kukutana na tayari wameanza kupitia mambo mbali mbali yanayofanywa  Katika huduma ya Usafirishaji na uchukuzi ili mtu aweze kutoka sehemu moja kwenda nyingine na mizigo au shehena au bidhaa ziweze kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni jambo ambalo linahusisha wadau mbali mbali. Yaani ni huduma moja inayotolewa na watu mbali mbali.

Amesema kuwa hasa katika kipindi hichi ambacho tumeingia uchumi wa kati ili tuweze kuimarika zaidi kwenda katika nchi zenye  uchumi wa kati wa juu  inabidi suala la usafirishaji na uchukuzi  tuongeze nguvu na juhudi na kuhakikisha kwamba kila mdau anatekeleza majukumu yake vizuri.

 Suala la usawa wa jinsia ni eneo ambalo limeanishwa vizuri kwenye mradi huo na chuo  kimetambua LHRC na kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kutuongezea maarifa sekta ya usafirishaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa amesema kuwa ushirikiano na taasisi hizo umekuja wakati muafaka ambao NIT inatekeleza miradi ya uboreshaji wa elimu (ESTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Amesema kupitia ushirikiano NIT itaweza kupiga hatua kwa kutatua  changamoto mbalimbali za kiutendaji na taasisi hizo anaamini kutakiwezesha chuo hicho kutimiza malengo yake ya kuzalisha wataalamu wenye umahiri hususani katika sekta ya usafirishaji.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha LHRC Hanna Henga alisema anaamini kupitia ushirikiano huo watakiwezesha chuo hicho kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ya elimu kwa uwiano sawa wa jinsia kwa wanafunzi na watumishi chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo cha Taifa Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa wakibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa Kituo cha TCDC, Sara Teri.
Mkuu wa Chuo cha Taifa Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza katika hafla ya kusaini  mkataba wa makubaliano  kati ya Kituo cha haki za binadamu na kituo cha TCDC leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa kituo cha TCDC, Sara Teri akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano kati ya NIT na TCDC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad