WAZIRI MKENDA ATUA BANDARI YA DAR ES SALAAM, AENDELEA NA MKAKATI WA KUDHIBITI ONGEZEKO LA BEI YA MBOLEA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 20, 2021

WAZIRI MKENDA ATUA BANDARI YA DAR ES SALAAM, AENDELEA NA MKAKATI WA KUDHIBITI ONGEZEKO LA BEI YA MBOLEA

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea katika bandari hiyo.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam leo Julai20, 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Msimamizi na ukisiaji wa ushushaji wa Mzigo ndani ya meli,  Asina Abdu akizungumza na waandishi wa habari wakati waziri wa Kilimo alipotembelea bandari ya Dar es Salaam leo Julai 20,2021 na kujionea shughuli ya upakuaji wa shehena ya mbolea katika bandari hiyo.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa serikali haina kodi kwenye mbolea ila sehemu pekee ya gharama ilikuwa ni ucheleweshaji wa kushusha mbolea pamoja na bei ya soko la Dunia. 

Hayo ameyasema leo Julai 20,2021 wakati wa ziara katika bandari ya Dar es Salaam na kuangalia namna meli zinavyoshusha shehena za mbolea. Amesema kuwa  mkakati wa serikali katika kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa wingi hapa nchini.

Amesema kuwa bei ya mbolea itashuka kwa viwango fulani kwani bei ya mbolea imepanda katika soko la dunia.

“Sijasema kwamba bei ya mbolea itashuka sana maana bei imepanda Duniani.” Amesema Prof. Mkenda

Waziri Prof. Mkenda amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mkakati wa kuhakikisha inadhibiti ongezeko la bei ya mbolea hapa nchini kwa Tanzania kwa kiasi kikubwa shughuli zake ni za Kilimo hivyo mbolea inatakiwa kuwa na gharama nafuu kwa Mkulima.

Amesema kuwa bei ya mbolea kwenye soko la Dunia imepanda kwa kiasi kikubwa hivyo serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa bei ya mbolea nchini inaendelea kuwa katika ustahimilivu wa bei huku juhudi zikiendelea za kuhakikisha bei ya mbolea inashuka bei.

Hata hivyo amewaasa wafanyabiashara wanaoficha mbolea kwaajili ya kuja kuuza badae bei ikiwa juu wazitie kwani serikali inamkakati wa kupunguza bei ya mbolea hapa nchini.

 “Hivyo natoa rai kwa wafanyabiashara wa mbolea nchini wanaohifadhi mbolea wakidhani bei itapanda, hilo hapana itashuka hivyo ni bora kuiuza mbolea hiyo mapem.a” Amewaasa Waziri Mkenda

Waziri Prof. Mkenda ameongeza kuwa Wizara yake tayari imefanya mazungumzo na Uongozi wa Bandari ya Dar es salaam ili kuhakikisha kuwa mbolea inapowasili bandarini inapewa kipaumbele ili iweze kupakuliwa kwa haraka na kuwafikia wakulima kwa wakati.

Licha ya hilo amepongeza  uongozi wa  Bandari ya Dar es salaam kwa kusimamia kwa ufasaha swala la upakuaji wa mbolea kwenye meli zinazowasili katika bandali hiyo ili iwafikie wakulima kwa wakati.

Hata hivyo Waziri mkenda amesema kuwa ili kuhakikisha changamoto za wafanyabiashara zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka tayari Serikali imeshatoa maelekezo ya Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) kuanza kutoa vibali vya kuuza mbolea ambayo imeshaingia nchini  badala ya vibali hivyo kutolewa ofisi ya Waziri wa Kilimo kama ilivyokuwa awali.

Ameongeza kuwa ili kuongeza ufanisi zaidi wa utendaji vibali hivyo vitatolewa kwa njia ya mtandao (Online) badala ya Ofisi ya Waziri wa Kilimo itakuwa na jukumu la kupewa taarifa ya utekelezaji wa utoaji vibali uliofanywa na TFRA.

Nae Kaimu Meneja wa kichele na uingizaji wa Mbolea pamoja na bidhaa nyingine, Tatu Moyo amesema kuwa mbolea inaendelea kuingizwa hapa nchini kufikia Julai 25,2021 meli nyingine inawasili hapa nchini itakuwa na tani elfu 11, vile vile Julai 29 meli itaingia hapa nchini itakuwa na mbolea tani elfu 4753 pia Julai 31 meli nyingine itawasili hapa nchini ikiwa na mbolea tani  efu 9400.

"Vile vile bandari ya Dar es Salaam katika kuendeleza kilimo kunameli imewasili hapa nchini imesheheni viwatilifu vya maji kwaajili ya kilimo imewasili hapa nchini leo Julai 20, 2021 asubuhi." Amesema Tatu

Tatu amesema kuwa meli nyingine itawasili mchana wa leo Julai 20, 20  ikiwa na kilo laki 306900 za salfa kwaajili ya uendelezaji wa kilimo hapa nchini.

Kwa Upande wake Msimamizi na ukisiaji wa ushushaji wa Mzigo ndani ya meli,  Asina Abdul ameiomba serikali, Wizara ya Uchukuzi kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuruhusu magari kupita katika vizuizi vyao kwani magari yenye mzigo wa mbolea yanapita katika barabara za Dar es Salaam.

"Tunaomba magari yaliyobeba mbolea yasiwe yanapita  TANROADS yawe yanapita moja kwa moja kwani wanaposimamishwa wanachelewa na inaleta usumbufu kwa madereva pamoja na tunaosafirisha mbolea." Ameomba Asina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad