Na Anthony Ishengoma –Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.Philemon Sengati amezitaka Halmashauri za
Shinyanga kutengeneza vikundi vya vijana wenye ujuzi na kuwajengea uwezo
kwa kuwapa kazi mbalimbali katika miradi inayoendelea katika
Halmashauri zao kama kama ambavyo Manispaa ya Kahama ilivyojenga uwezo
kwa vikundi hivyo na kuvipa kazi katika jengo jipya la utawala ambalo
lipo katika hatua za mwisho kukamilika.
‘’Wakati mkiwa katika
hatua za kutayarisha vikundi hivyo na kuvijengea uwezo endeleeni kutoa
kazi vikundi hivi vya Manispaa ya Kahama katika miradi yote inayoendelea
katika Halmashauri za Shinyanga na hili ni agizo la viongozi wa
Mkoa.’’Aliongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema hayo alipofanya ziara Wilaya ya Kahama na kujionea
maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa ya Kahama na
kushuhudia vijana wazawa ambao walisanifu michoro ya jengo na kusimamia
ujenzi ikiwemo kupewa kazi ya kuweka thamani katika jingo hilo jipya
lenye ubora.
Aidha Dkt. Sengati ameshauri Manispaa ya Kahama
kuendelea kuwajengea uwezo wazawa na kutangaza kazi zao ili waweze
kupewa kazi hata katika Nchi jilani ili kuweza kuiletea sifa Tanzania
kwani wamefanya kazi nzuri sana kama zile ambazo kwa kawaida zimekuwa
zikifanywa na wakandarasi wa kigeni.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga Dkt. Batlida Buriani aliwapongeza viongozi wa Manispaa ya
Kahama kwa kuwaamini Wahandisi wa kike ambao walisanifu michoro ya jengo
na kusimamia ujenzi wa jengo hilo la kisasa tofauti na wengine ambao
wangetoa kazi hiyo kwa watu wengine ikiwemo raia wa kigeni.
‘’Katika
hali ya kawaida ya mfumo dume isingekuwa raisi kwa nyinyi kuwaamini
mabinti awa lakini nyie mumekwenda mbele zaidi na kuwapa fursa na kila
atakeye kuja nakuoneshwa kuwa ni awa wamefanya kazi hii hakuna
atakayeamini na hii itatoa fursa kwa mabinti wengine walioko vyuoni
kuiga mfano huu’’. Aliongeza Dkt. Batlida Buriani Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga.
Dkt. Buriani aliongeza kuwa katika uongozi wake
ataangalia namna ya kuwashirikisha wanawake zaidi katika miradi ili
kufikia malengo endelevu ya kuwaezesha wanawake kiutalaam lakini pia
kiuchumi.
Mhandisi msamimizi wa Jengo hilo Bi. Immaculata Chaula
meviambia vyombo vya habari kuwa alijifunza utaalaam wa masuala ya
ujenzi katika Chuo Cha Teknolojia Kilichopo Mbeya (MUST) lakini pamoja
na kupata taaluma yake hiyo ni ushiriki wake katika kusimamia moja ya
ukumbi wa Manispaa hiyo ndio ulipelekea kumwami na kumpa kazi hiyo.
Bi.
Chaula aliongeza kuwa baada ya kumaliza masomo yake alianza kuomba kazi
kama fundi wa kawaida mitaani na taaluma yake inachangia sana katika
ufanisi wa kazi zake na hivyo kuweza kuaminiwa kwa kazi kubwa
anayoifanya kwa sasa.
Jengo la kisasa linalojengwa kwa mfumo wa
akaunti ya dharula linajengwa kwa mapato ya ndani na mpaka sasa lipo
katika hatua za mwisho kukamilika tayari kwa matumizi ya ofisi ya
watumishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Kataibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Batlida Buriani wakifuatilia kwa makini ujenzi wa jengo jipya la Utawala la Manispaa ya Kahama jana walipotembelea jengo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Batlida Buriani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Manispaa ya Kahama na wasanifu majengo wa jengo hilo jana walipotembelea jengo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi wa jingo hilo.
No comments:
Post a Comment