Mkuu wa biashara wa Equity Group Polycap Igathe pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Bank (T) Esther Kitoka Wakionesha mfano wa kadi mpya ya "Eazzy Card" iliyo zinduliwa na benki hiyo Dar es Salaam. 22 June, 2021
Mkuu wa biashara wa Equity Group Polycap
Igathe (kushoto) akishika kadi mpya "Eazzy Card" pamoja na viongozi
wa Equity Bank (T) katika uzinduzi wa kadi hiyo mpya ya malipo uliofanyika Dar
es Salaam. 22 June, 2021
Dar Es Salaam Tanzania, 22 June, 2021– Benki
ya Equity (T) leo wamezindua rasmi
kadi ya malipo ya awali ijulikanayo kama
“Eazzy card” ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya kiditali na nchini kupitia
huduma za fedha jumuishi.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika
katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Bank (T) Esther Kitoka alisema, kuwa kadi
hiyo ni ya malipo ya kabla, ambapo mmiliki anaweza kutumia kiasi cha fedha
ambacho tayari amekiingiza na kukitunza katika kadi yake husika. “Kadi hii ni ya malipo ya awali hivyo inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo kulipia ankara au bili, kununua bidhaa, kutoa pesa kwenye mashine
za ATM na pia kufanya malipo ya mtandaoni.”
Pia ameeleza kuwa watanzania wengi wameonesha
hamasa ya malipo ya kidigitali hivyo watahakikisha kuwa huduma hizo za kufanya
malipo kwa njia ya mtandao zinawafikia wateja wao na wana malengo makubwa
mbeleni katika kujenga uchumi wa nchi hasa kwa kwa kuzingatia sera ya
nchi kwa sasa inayohamasisha na kuongeza kasi ya ukuaji wa malipo kwa njia ya
kadi.
Akizungumzia
juu ya faida ya kadi hizo Kitoka alisema kuwa zinamuongezea
mteja au asiye mteja Benki ya Equiy uwezo
wa kufanya manunuzi pasipo kuwa na haja
ya kubeba pesa taslimu. “Kuzipata kadi hizi sio lazima uwe mteja wa Benki ya
Equity, pia ni rahisi kuziongezea salio kwa kupitia Wakala, Simu za Mikononi,
matawini na kupitia huduma fedha kwa njia ya simu” alisema.
Naye Mkuu wa kitengo
cha Malipo na Huduma mbadala wa benki hiyo Raph Ligalama ameeleza kuwa lengo
la uzinduzi wa kadi hiyo ni pamoja na kurahisisha na kuwawezesha wateja na wasio wateja wao kufanya
(miamala) kidijitali na hivyo kuwaondolea usumbufu.
Faida za Eazzy card kutoka Equity Bank
·
Rahisi
kufungua (Unahitaji kitambulisho cha NIDA tu)
·
Hakika
na salama
·
Imeunganishwa
na mtandao wa Visa hivyo kuweza kutumika kokote duniani
·
Urahisi
wa kufanya malipo kwenye maduka, vituo vya mafuta, mahosipitali Daladala na masokoni.
·
Huondoa
ulazima wa kubeba fedha taslimu hivyo kupunguza hatari ya wizi au mahitaji ya
chenji.
·
Rahisi
kujaza fedha
·
Inatumia
kokote duniani
·
Uwezo
wa kuchukua pesa taslimu inapobidi (kupitia Wakala, ATM au tawi)
·
Uwezo
wa kufanya malipo ya mtandaoni
No comments:
Post a Comment