USAILI WA WANAMITINDO KUELEKEA LADY IN RED WAFANYIKA DAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 30, 2021

USAILI WA WANAMITINDO KUELEKEA LADY IN RED WAFANYIKA DAR

 


Mmoja ya washiriki akipima urefu ikiwa ni moja ya kigezo cha ushiriki wa tamasha la 'Lady in Red' litakalofanyika Februari 13 katika hoteli ya Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.
Majaji wa jukwaa la Lady in Red lililoandaliwa na mkongwe wa tasnia ya ubunifu nchini bi. Asia Khamsin wakiwa wakiwa tayari kwa kazi, leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakiendelea kufanya usaili.

USAILI wa  kusaka wanamitindo  watakao pamba tamasha la 'Lady in Red' litakalofanyika  February 13 umefanyaika leo Masaki Elements jijini Dar es Salaam huku vijana wengi wakijitokeza kuonesha ubunifu wao ili kuweza kupata fursa zaidi katika masuala ya urembo, mitindo na ubunifu.

Tamasha hilo ambalo linafanyika kila mwaka mwezi wa pili kwa ajili ya kuinua vipaji vya wabunifu kwa kuonyesha kazi zao na kwa mwaka huu linafanywa na kampuni ya Hugo Domingo pamoja na chama cha wabunifu nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari muasisi wa onyesho hilo Asia Idarus Khamsini, 'Mama wa Mitindo,' amesema mwaka  tamasha hilo litafanyika katika ubora wa juu kuliko miaka iliyopita na kusema kuwa mwitikio kwa mwaka huu ni mkubwa ukilinganisha na miaka mingine.

"Tokea nistaafu kuandaa tamasha la 'Lady in Red' limeshuka kiwango chake lakini mwaka huu tumepata waendeshaji ambao wana kiu ya kuinua tasnia yetu hivyo litakuwa ni tamasha lenye hadhi ya kimataifa," amesema mama wa Mitindo.

Aliongeza kuwa mpaka sasa wabunifu  wengi wamejisajili kwa  kuonyesha kazi zao siku hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Usaili huo umeendeshwa na wataalamu na wabunifu wakubwa wa mavazi akiwemo Martin Kadinda, Ally Rhemtura na Mustapha Hasanali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad