NMB yatoa msaada wa vifaa vya hospitali Tarime vijijini, Ushetu, Mikumi na Madawati Ndanda - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 15, 2020

NMB yatoa msaada wa vifaa vya hospitali Tarime vijijini, Ushetu, Mikumi na Madawati Ndanda

 

 Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali; vitanda, magodoro na mashuka vyenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano kwa hospitali za halmashauri za wilaya za Tarime vijijini (Mara), Ushetu katika wilaya ya Kahama (Shinyanga) na Mikumi - wilaya ya Kilomero (Morogoro). 


Vifaa hivyo vimekabidhiwa wakati Benki hiyo ikizindua huduma mpya tatu za kibabe katika maeneo mbali mbali nchini; Namba ya WhatsApp 0747333444, njia ya digitali ya kutoa maoni kwa mfumo wa kuscan QR pamoja na mfumo wa kurudisha token za umeme (token retrieval) wakati wakiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. 

Hospitali mpya ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime iliyopo Nyamwanga ilikabidhiwa vitanda saba vikiwemo viwili vya kujifungulia na magodoro. Akipokea msaada huo Katibu Tawala wa wilaya ya Tarime, John Marwa alisema msaada huo utaboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya watu 300,000 wakiwemo wamama wajawazito.Mkuu wa Mauzo – Idara ya Hazina ya Benki ya NMB, Jeremiah Lyimo (wapili kutoka kushoto) akikabidhi msaada wa vitanda saba vikiwemo viwili vya kujifungulia na magodoro kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime - John Marwa, watatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Apoo Castro Tindwa, Meneja wa NMB Tawi la Nyamongo, Erick Manyama (mwenye miwani) pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Baraka Ladislaus. 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama - Anamringi Macha (mwenye Miwani) akipokea msaada wa vitanda, magodoro na mashuka kutoka kwa Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB - Emmanuel Akonaay kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Ushetu - Kahama.

Mwanasheria Mkuu wa Benki ya NMB, Lilian Komwihangiro akimkabidhi magodoro na vitanda kwa Katibu Tawala wilaya ya Kilosa, Yohana Kastila (kulia) kwa ajili ya kituo cha afya Mikumi. kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kilombero, Rehema Nassibu na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki hiyo, Dismas Prosper. 

Katika hatua nyingine, Benki hiyo pia imetoa msaada wa meza na viti 50 kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Mkalapa iliyopo Ndanda wilaya ya Masasi, ili kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Masasi, Selemani Mzee (kulia), akipokea msaada wa meza na viti 50 kutoka kwa Afisa Mkuu wa Udhibiti Hatari na Utekelezaji wa Benki ya NMB, Victor Rugeiyamu, kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mkalapa, wilayani Masasi - mkoani Mtwara. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango. 

Benki ya NMB kupitia kitengo chake cha Uwajibikaji kwa Jamii, imekua na utaratibu wa kurejesha sehemu ya faida yake ya asilimia moja kwa jamii kusaidia katika sekta ya afya, elimu na majanga. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad