DKT MAGUFULI ACHUKUA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUGOMBEA KITI CHA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO JIJINI DODOMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 6, 2020

DKT MAGUFULI ACHUKUA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUGOMBEA KITI CHA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO JIJINI DODOMAMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles na Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk. Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25,2020. (Picha na NEC).
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mgombea Mwenza,Mhe Samia Suluhu Hassan begi lenye fomu za kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania,katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage,Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles na Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Mwenza,Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha begi lenye fomu za kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania,katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akizungumza jambo kabla ya kukabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.

Mgombea Mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha Mahudhurio katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) akisaini kitabu cha Mahudhurio huku Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles akishuhudia kabla ya kukabidhiwa fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono baadhi ya Wageni waliofika eneo hilo leo mara baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera Charles akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya fomu za kugombea kiti cha Rais Kwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. John Pombe Magufuli katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad