Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amemtaka Mkandarasi
wa Kampuni ya NAMIS CORPORATE L.T.D ambaye anajenga Soko hilo kuongeza kasi ya
ujenzi huo ili Wafanyabiashara waweze kurudi kwenye eneo lao.
Mhe. Chongolo amesema hayo alipofanya ziara katika soko la
Tandale na kuwakuta wafanyabiashara katika mazingira yasiyo rafiki hali
inayopelekea usumbufu wa shughuli zao na
kumuelekeza mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi huo ili kuondokana
na adha inayowakabili.
Amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundo mbinu yote
ya masoko ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara na kuendesha maisha yao
na hivyo kuziwezesha Halmashauri kufikia malengo hayo.
Amefafanua kuwa mradi huo wa Soko la kisasa unajengwa kwa
gharama ya Sh. Bilioni 8.7 fedha ambazo zimetolewa na Serikali kuu na kwamba tayari
mkandarasi huyo ameshalipwa fedha
zote na hivyo kusisitiza kwamba anapaswa
kufanya kazi usiku na mchana ilikukamilisha kazi yake kwa wakati.
“Serikali ya Rais Dk.
John Magufuli imemlipa mkandarasi pesa zote, hivyo hatudai badala yake sisi
ndio tunamdai Soko letu atukabidhi kwa wakati sahihi, wafanyabishara na
wananchi wanasubria kwa shauku kubwa sana ukizingatia Soko hili nimuhimu kwa
wakazi wa Dar es Salaam, kwasababu litahusika zaidi na biashara ya mazao ya
nafaka pamoja na bidhaa nyingine” amesema Chongolo.
Awali Meneja kutoka kampuni hiyo iliyopewa kandarasi ya
ujenzi wa Soko hilo Mhandisi James Msumari alimueleza Mhe. Chongolo kuwa ujenzi
huo utachukua miezi 12 jambo ambalo alionesha kutokuridhishwa na muda huo na
kusema kuwa hakuna sababu ya kutumia
muda mrefu kwakuwa fedha wanazo hivyo wanapaswa kukamilisha ujenzi kwa makubaliano
yaliyoingiwa.
Kwaupande wake Mhandisi Msumari amesema wamepokea maagizo na
wako tayari kuyatekeleza ili waweze kuondoa changamoto zinazowakabilio
wafanyabiashara wa eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo
akitoa maelekezo kwa Meneja mradi wa Kampuni ya ujenzi NAMIS CORPORATE
L.T.D Mhandisi James Msumari mara baada
ya kukagua mradi wa ujenzi wa soko hilo.
Muonekano wa soko la Tandale linaloendelea kujengwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo
akipata maelezo kutoka kwa Meneja mradi wa Kampuni ya ujenzi NAMIS CORPORATE
L.T.D Mhandisi James Msumari namna ambavyo Soko hilo litakavyokuwa.
Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akipata maelezo ya ujenzi wa Soko la Kisasa
la Tandale kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa, Mhandisi Mkerewe Tungaraza kabla ya
kuanza kukagua soko hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo
akikagua ujenzi wa Soko la kisasa la Tandale leo wakati alipofanya ziara ya
ukaguzi wa soko hilo wenye lengo la kujionea namna ambavyo ujenzi huo
unavyokwenda.
No comments:
Post a Comment