WAZIRI MKUU ASEMA KESHO SIKU YA KUAGA KITAIFA MWILI WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA, WATANZANIA TUJITOKEZE KWA WINGI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 27, 2020

WAZIRI MKUU ASEMA KESHO SIKU YA KUAGA KITAIFA MWILI WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA, WATANZANIA TUJITOKEZE KWA WINGI

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Watanzania tumeendelea kupeana pole ,tuko kwenye majonzi na imeshatangazwa tuko katika maombolezo huku akitumia nafasi hiyo kueleza baada ya jana na leo wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kesho itakuwa ni siku ya kitaifa.

Akizungumza leo jioni uwanjani hapo Waziri Mkuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Kitaifa ni kwamba kesho itakuwa ni siku ya viongozi ambao hawakupata nafasi ya kuaga katika siku mbili ndio watakaopata nafasi hiyo wakiongozwa na Rais Dk.John Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Ali Shein ,viongozi wa nchi jirani au wawakilishi wao ,viongozi wa dini na viongozi wengine kwa mujibu wa utaratibu.
"Viongozi, wananchi na marafiki wa nchi jirani wataungana nasi  siku ya kesho ambayo tunaaga kitaifa na baada ya kuaga mwili utapelekwa Lupaso.Wananchi wa Lupaso nao watapata nafasi ya kuaga kuanzia saa mbili na nusu mkapa saa saba na baada ya hapo mwili utapumzishwa.Watanzania wameonesha upendo mkubwa kwani wamejitokeza kwa wingi kuaga mwili wa mzee wetu,"amesema Waziri Mkuu.

Hata hivyo amesema kupitia vyombo vya habari, watanzania wa kada mbalimbali pamoja na viongozi kila mmoja ameelezea mambo mengi makubwa yaliyofanywa na Rais mstaafu Mkapa."Rais mstaafu Mkapa amefanya mambo mengi,wengi wameeleza sina sababu ya kurudia." Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru waandishi wa habari, vyombo vya ulinzi na usalama na kila Mtanzania kutokana na ushiriki wao katika kipindi hiki kigumu.
Waziri Mkuu ameendelea kuhamasisha wananchi wote kushiriki siku ya kesho na ratiba itaanza saa nne kamili na itachukua saa mbili na kama muda utaongezeka basi itakwenda mpaka saa saba."Ratiba itaanza saa nne kamili asubuhi hadi saa sita mchana kama itaongezeka basi haitafika saa saba."

 Wakati anatoa maelezo hayo, Waziri Mkuu alikuwa ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiaga Mwili wa Marehemu Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Leo Julai 27, 2020 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad