HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 1, 2020


NMB Kenyatta 
NMB Clock Tower

NMB Madaraka 

NMB Bank House


Meneja Uhusiano Mwandamizi wa NMB Kanda ya Kaskazini anayeshughulikia Kilimo- Oscar Rwechungura alisema katika kuadhimisha Wiki ya Maziwa kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya maziwa wanawezesha sekta hiyo katika mnyororo wa thamani. 

“NMB inawezesha sekta hii kuanzia ngazi ya mwanzo kwa wafugaji wenyewe, wafanyabiashara wa dawa za mifugo na wasindikaji wa mazao ya maziwa katika kuhakikisha tunaimarisha sekta nzima ya maziwa na kuimarisha afya za watumiaji wakiwemo wafanyakazi wa NMB,” alisema Rwechungura 

Alisema lengo la NMB ni kupanua wigo kwa wafugaji wadogo ili waweze kupata huduma za kifedha kwa njia rahisi ili kuongeza idadi ya ng’ombe, vyakula vya mifugo na huduma za matibabu ya mifugo ili kuongeza tija ya ufugaji wao. 

“Lengo letu ni kuwawezesha wazalishaji wa maziwa kuongeza tija,badala ya mfugaji kutegemea kupata maziwa lita mbili kwa siku jambo ambalo halimfanyi aone faida ya kazi anayoifanya tunatamani apate lita 20 na zaidi kwa siku hivyo ili mfugaji apate faida lazima aongeze matumizi kwa kupata uwezeshwaji kutoka kwetu,” 

NMB haishii kuwawezesha wafugaji wadogo na kati kupata mitaji pekee bali inawaunganisha na masoko ili kuwezesha mnyororo wa thamani katika sekta nzima ya maziwa kuanzia kwa mfugaji hadi anayepeleka maziwa sokoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad