HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 7, 2020

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MBEGU ZA MAHINDI KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, sehemu ya mbegu za mahindi tani nne zenye thamani ya shilingi milioni 20 zilizotolewa na Benki hiyo kupitia ombi maalum la Mbunge wa Kuteuliwa anayewakilisha mikoa ya Lindi na Pwani na Mwenyekiti wa mfuko Wanawake na Maendeleo Foundation (WAMA), Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mkoa huo ambao mashamba yao yaliathiwa na mafuriko mapema mwaka huu. Makabidhiano hayo yamefanyika Aprili 5, 2020 kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mjini, Shaibu Ndemanga na kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kusini, Jenipher Tondi. Aidha Mkuu wa Mkoa aliishukuru Benki ya CRDB kwakuwa mastari wa mbele katika kutatua matatizo ya wananchi sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mkoani Lindi kwani hapo awali CRDB Benki kupitia tawi lake la Lindi iliweza kuwasaidia wahanga hao kwa kuwapatia Magodoro, mashuka, nguo, Chakula nk.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (katikati) akionyesha sehemu ya mbegu za mahindi tani nne zenye thamani ya shilingi milioni 20 zilizotolewa na Benki ya CRDB kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Tully Esther Mwambapa (wa pili kulia) kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mkoa huo ambao mashamba yao yaliathiwa na mafuriko mapema mwaka huu. Mbegu hizo zilipatikana kupitia ombi maalum la Mbunge wa Kuteuliwa anayewakilisha mikoa ya Lindi na Pwani na Mwenyekiti wa mfuko Wanawake na Maendeleo Foundation (WAMA), Mama Salma Kikwete (wa pili kushoto), ambaye alilipata kutoka kwa wananchi mbalimbali walioathirika na mafuriko pindi alipowatembelea. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mjini, Shaibu Ndemanga na kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kusini, Jenipher Tondi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (katikati) azungumza kabla ya kupokea sehemu ya mbegu za mahindi tani nne zenye thamani ya shilingi milioni 20 zilizotolewa na Benki ya CRDB kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Tully Esther Mwambapa (wa pili kulia) kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mkoa huo ambao mashamba yao yaliathiwa na mafuriko mapema mwaka huu, ikiwa ni ombi maalum la Mbunge wa Kuteuliwa anayewakilisha mikoa ya Lindi na Pwani na Mwenyekiti wa mfuko Wanawake na Maendeleo Foundation (WAMA), Mama Salma Kikwete ambaye alilipata kutoka kwa wananchi mbalimbali walioathirika na mafuriko pindi alipowatembelea.
 Mbunge wa Kuteuliwa anayewakilisha mikoa ya Lindi na Pwani na Mwenyekiti wa mfuko Wanawake na Maendeleo Foundation (WAMA), Mama Salma Kikwete akizungumza wakati akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad