HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 24, 2020

NBC YAZINDUA KLABU YA BIASHARA TANGA, YATOA MAFUNZO YA KIBIASHARA.

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Maheji ameipongeza Benki ya NBC kwa kuamua kufungua klabu na kutoa elimu ya mlipakodi, utunzaji wa kumbukumbu na jinsi ya kuweka mahesabu sawa. 

Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa Klabu ya NBC B Club iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii.

“Niipongeze Benki ya NBC kwa uzinduzi wa klabu hii na kutoa mafunzo haya kwani moja ya eneo 
ambalo wafanyabiashara wengi wanakosa ni hili la utunzaji wa taarifa za biashara zao yaania 
kumbukumbu, hivyo niimani yangu kuwa litapunguza sana migogoro kati ya wafanyabisha na Serikali hasa TRA wakati wa ukadiriaji wa kodi zao’ amesema Maheji. 

Benki hiyo imezindua klabu ya biashara Katika mkoa wa Tanga yenye Lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati pamoja ili kupeana 
fursa, mbinu na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusi biashara zao. 

Katika uzinduzi huo, NBC wameendesha mafunzo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati kwa lengo pia la kuwaongezea uwezo, uelewa na ubunifu katika ufanyaji wa 
biashara zao. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Klabu hiyo ya Biashara mkoani Tanga, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NBC, Elvis Ndunguru amesema kuwa benki hiyo imedhamiria kurahisisha huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali hususani wafanyabiashara ambao ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini. 

Amesema kuzinduliwa kwa klabu hiyo ya Biashara kunafanya klabu za biashara katika benki 
hiyo nchini kuwa malengo yake ni kuwaunganisha na kuwakutanisha wafanyabishara pamoja ili kutafuta fursa za ufanyaji wa biashara na kubadilishana uzoefu. 

Ndunguru amesema klabu hizo za biashara zimekuwa sehemu ya wafanyabiashara kupata 
masoko na kuongeza kuwa katika kuhakikisha benki inachangia ukuaji wa sekta ya biashara 
nchini, imeamua kuanzisha vilabu hivyo vya wafanyabiashara (NBC B Clubs) ili kukuza na 
kuimarisha biashara nchini. 

"NBC B Club ni mahali muafaka pa kuelimisha wafanyabiashara juu ya masuala mbalimbali 
kuhusu biashara na tangu kuanzishwa kwa klabu hizi za biashara, wanachama wamekuwa 
wakinufaika na mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia vitabu vya mahesabu, elimu ya 
masoko na pia elimu ya mlipa kodi kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA," 
amesema na kuongeza. 

"Klabu hizo zimekuwa zikipanua masoko kwa wafanyabiashara, kwa mfano kwa miaka 
minne mfululizo sasa tumekuwa tukipeleka wafanyabiashara China na mwaka huu 
tunatarajia kuwapeleka Ujerumani kwa sababu kuna maonesho ya viwanda lakini pia 
tunafikiria kupeleka watu Ulaya na Marekani kwa ajili ya kukutana na wenye viwanda na 
wanaotengeneza mashine mbalimbali jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wetu," 
alisema 

Kwa upande wake Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka TRA makao makuu, Julius Mjenga 
amesema wafanyabiashara wanapaswa kuwa makini katika kutunza kumbukumbu za biashara 
ili kuepusha migororo na TRA hasa wakati wa ukadiliaji wa kodi. 

"Napenda kuwaambia wafanyabiashara kwamba ili waweze kukadiliwa kodi zao vizuri ni 
muhimu watunze kumbukumbu zao, hata hivyo changamoto kubwa inayoonekana kati ya 
TRA Na wafanyabiashara ni kulalamikia makadirio ya kodi sasa ili hii iondoke watunze 
kumbukumbu zao," amesema.

Naye Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Tanga, Liberat Macha 
amesema wamekuwa walitoa mikopo kwa wajasiriamali wanaoanza na kuendelea na biashara hivyo watu wasisite kuja kuchukua kwani vigezo ni kuwa na mradi halali unaoendeshwa kwa mujibu wa utaratibu unaotambulika kisheria. 


Kwa upande wake mfanyabiashara ambaye ni mteja wa NBC aliyenufaika na klabu za biashara, Haji Mambo amesema kupitia klabu hizo wameweza kuunganishwa na watu mbalimbali duniani ambapo yeye alifanikiwa kwenda China na kuonana na wafanyabiashara wengine waliombadilisha mawazo na mitazamo katika biashara zake. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanga, Daudi Mahej (Wa pili kulia), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru kuashiria uzinduzi rasmi wa Club ya biashara katika Mkoa wa Tanga (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa wadogo na wakati wa NBC Evance Luhimbo pamoja na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Tanga Asia Chambega. Uzinduzi huo umefanyika Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Halmashauli ya jiji la Tanga Daudi Mahej akifafanua jambo kwa maofisa wa Benki ya NBC, baada ya kuzindua rasmi mafunzo ya wafanya Biashara wadogo na wakati yalioandaliwa na Benki ya NBC (kulia) ni Mkuu wa Kitengo cha Benki ya Kiislam Nbc Mohamedi Nuh (Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wakati Evance Luhimbo, pamoja na Meneja wa NBC tawi la Tanga Asia Chambega
Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru akishikana mikono na Afisa Mkuu Msimamizi wa kodi TRA makao makuu, Julius Mjenga baada ya kumaliza mafunzo ya yabiashara yalioandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanya Biashara wa Mkoa wa tanga mwengine pichani ni Meneja Uhusiano Benki ya NBC William Kallaghe
Mkurugenzi wa Idara ya Wafanya Biashara wa Benki ya NBC Elvis Ndunguru akizungumza wakati wa Mafunzo ya Biashara kwa wafanya Biashara wadogo na wakati wa Mkoa wa Tanga wakati wa Uzinduzi wa Club ya Biashara mkoani tanga hafla ya uzinduzi huo umefanyika jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad