Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB agawa chai kwa wateja - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 7 October 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB agawa chai kwa wateja

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amewaongoza baadhi ya watendaji wa benki hiyo kugawa chai kwa wateja wao.

Akizungumza akiwa kwenye tawi la Kariakoo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Nsekela alisema ni wiki muhimu kwa wateja wa CRDB.

Alisema ni wiki ya viongozi wa benki hiyo kutoka matawi yote kuwafuata na kuwahudumia wateja kwa upendo chini ya kaulimbiu ya 'Ulipo tupo kukupa Magic'.

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani kaulimbiu ya dunia ni 'The magic of service' na sisi benki yetu tunashiriki kwa kuwahudumia wateja wetu.

"Tunawaambia ulipo tupo kukupa Magic. Tumeandaa vitu vingi vizuri naamini wateja wetu watafurahia," alisema Nsekela.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifungua Shampeni kuashiria kuanza kwa wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa sehemu mbalimbali duniani, katika hafla iliyofanyika kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimiminia Shampeni  mmoja wa wateja wa Benki hiyo, waliofika kupata huduma kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad