MATUKIO KATIKA PICHA: MKUTANO WA WAWEKEZAJI, WAFANYABIASHARA – MTWARA, LINDI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 26 September 2019

MATUKIO KATIKA PICHA: MKUTANO WA WAWEKEZAJI, WAFANYABIASHARA – MTWARA, LINDI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki, Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (katikati) na Waziri wa Madini Doto Biteko wakielekea kwenye mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa (katikati) na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (kushoto) wakifuatilia hoja mbalimbali za wafanyabiashara na wawekezaji wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Lindi. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Mbunge wa Mtwara vijijini Hawa Ghasia akichangia jambo wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Mfanyabiashara wa matunda mkoani Mtwara Hamis Mfaume akieleza changamoto zinazomkabili katika biashara yake wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani humo.
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoani Lindi, Mariam Mfunda akieleza changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu katika shughuli zao za uzalishaji wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani humo.
Meneja wa Usajili wa Walipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu, Rehema Shao akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad