HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 28, 2019

WAKULIMA WA ZAO LA MUHOGO MKURANGA WAPATA KIWANDA CHA KUCHAKAZA MUHOGO

VICTOR MASANGU, MKURANGA
KILIO cha muda mrefu ambao kilkuwa kinawakabili wakulima wa zao la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani hatimaye hivi karibuni wanatarajia kuondokana na changamoto sugu ya upatikanaji wa soko la uhakika kufuatia kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo ambacho kitagharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.5

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakulima hao wakati wa Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa halfa ya uwekeaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho ambacho kimejengwa na mwekezaji kutoka nchini China katika kijiji cha Mkenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga ambapo wamedai hapo awali walikuwa na tatizo la kuuza mihogo yao kwa bei ya hasara.

“Sisi kama wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilayah ii ya mkuranga tumefarijika sana kwa ujio wa mradi w akiwanda hiki ambacho kimejengwa na marafiki zetu wa kutoka nchini chini, na tunashukuru kwa jitihada ambazo zinafanywa na Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais wetu Dk. John Pombe Magfuli kwa kuwaleta wawekezaji hawa ambao watatusaidia kuondokana na tatizo la kupata soko la uhakika,”walisema wakulima hao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka maafisa kilimo wote kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwasimamia vema wakulima wa zao hilo la muhogo kutonyonywa na walanguzi na kupata haki zao stahiki na kuahidi kuwaondoa kazini wale wote ambao watabainika kukwamisha juhudi za serikali katika uwekezaji sekta ya viwanda.

Aidha Ndikilo alisema kuwa lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawasaidia kwa hali na mali wananchi wake katika kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ikiwemo ukosefu wa masoko ya ukakiha, ajaira hivyo aatahakikisha zao hilo la muhogo linapata soko kupitia viwanda ambavyo vinajengwa na waekezaji katika maeneo mbali mbali na kuwahimiza wasikate tama na badala yake waendelee zaidi kulima mazao ya biashar ikiwemo ufuta,muhogo na korosho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amesema kuwa kipindi cha nyuma wakulima wengine walikuwa tayari wameshakata tamaa katika kilimo cha zao la muhogo,hivyo kumamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kuleta mabadili chanya kwa kuwapa fursa wananchi kuwa na soko la uhakika .

“Kwa kweli wananchi wangu hasa kwa wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga baadhi yao walikuwa tayari wameanza kukata tama kabisa na kujikitza zaidi na kilimo cha zo la muhogo nah ii hali ni kutokana na mfumo ambao ulikuwepo wanauza mazao yao kwa bei ya hasara kweli lakini kwa sasa kiwanda hiki kinakamilika mwaka huu hivyo wataondokana kabisa na changamoto ya soko,”alismema Sanga.

Awali akisoma Risala ya ujenzi wa mradi huo mmoja wa vongozi wa kiwanda Leonard Jambeli kwa niaba ya Mkurugenzi amebainisha kwamba waanategemea kutoa fursa za ajira za moja kwa moja kwa wazawa zaidi ya mia moja pindi uzalishaji utakapoanza kufanyika rasmi.

KUKAMILIKA kwa mradi huo wa ujenzi wa kiwanda mwishoni mwa mwaka huu kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa zao hilo katika halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ambao kwa miaka mingi walikuwa wanapata hasara kutokana na kunyonywa na walanguzi kununua zao hilo kwa bei ndogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo kushoto akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo mara baada ya halfa ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho amabcho kimejengwa katika kijiji cha Mgenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga,(PICHA NA VICTOR MASANGU)
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani kushoto Mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata muhogo wakati alipofanya ziaara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa kaatika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbali mbali wa kiwanda hicho cha kuchakata muhogo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi.
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kushoto Ramadhani Maneno akimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ikiwa ni moja ya ishara ya kumpongeza katika juhudi zake za kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa viwanda
  Mmoja wa viongozi wa kiwanda hicho cha kuchakata zao la muhogo kulia Leonard Jambeli akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho pembeni yake kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na baaadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na watumishi mbali mbali wa serikalini, pamoja na wananchi wa wa kijiji cha Mkenge hawapo pichani katika halfa fupi iliyoandaliwa kwa lengo la uwekezaji wa jiwe la msingi kataika kiwanda hicho.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad