HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 23, 2019

WATEJA WA ZANTEL KUPATA SAA MOJA YA DATA BURE KWA MIEZI 3

Kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imezindua kampeni mpya ambayo itawawezesha wateja wake kutumia bure huduma za data kwa saa moja kila siku kwa kipindi cha miezi mitatu, ikiwa ni utekelezaji wa dhamira yake ya kuwapa motisha wateja wake kwa kuwapatia huduma bora za intaneti yenye kasi kubwa.

Kampeni hiyo inayojulikana kama 'Msako Time'ni kwa ajili ya wateja wote nchi nzima upande wa Visiwani na Bara. Wateja wa Zantel wataweza kutumia huduma ya intaneti bure, kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 10 jioni kila siku kuanzia leo.

Kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa Zantel kuwapatia motisha wateja wake na kuwahimiza kutumia huduma ya data za mtandao wake na kujionea huduma za intaneti yenye kasi kubwa isiyo na kikomo.

“Tunazo huduma madhubuti za intaneti zinazoongoza kwa ubora katika soko, hii inatufanya kuwa na ujasiri wa kuwapatia fursa wateja wetu kupata uzoefu wa kutumia intaneti ya mtandao wetu. Kupitia kampeni hii tumelenga pia kuwapatia motisha wateja wetu kutokana na kuendelea kutuamini na kutumia huduma zetu za data,” amesema Mkuu wa Huduma na Upangaji Bei wa Zantel, Aneth Muga.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Kisonge Zanzibar, Muga alifafanua kuwa, kupitia kampeni ya ‘Msako Time’, wateja wa Zantel watakaonunua kifurushi kabla ya saa tisa mchana watapata ofa ya ‘saa moja ya kufurahi’ kwa kutumia bure huduma za intaneti.

“Ofa hii ni kwa ajili ya wateja wanaotumia mtandao wa Zantel na wateja wapya watakaojiunga na Zantel. Ili kupata ofa hii kinachotakiwa ni kuunua kifurushi cha data cha shilingi 1,000/- au zaidi kiwe cha siku, wiki au mwezi baada ya hapo watazawadiwa saa moja bure ya  kutumia na kufurahia intaneti ya  BURE. Ofa hii kupitia kampeni ya 'Msako Time' itakuwa  inapatikana  kila siku kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa kumi jioni, hii inamanisha katika muda huo hawatakatwa gharama za matumizi ya data kutoka kwenye vifurushi walivyonunua badala yake watapata huduma za kutumia data bure,”aliongeza.

Kampeni hii ya data inadhihirisha dhamira ya Zantel kuendelea kutoa huduma za gharama nafuu za intaneti zenye kiwango cha juu cha ubora na inavyoendelea kuwekekeza kufanikisha jambo hilo. 

Katika mradi wake wa kuboresha mtandao wake wa hivi karibuni, Zantel imesambaza huduma zake katika mikoa 22 ya Tanzania na mtandao wake unapatikana kwa kasi kubwa na kiwango cha juu cha ubora, umesambaa kwa asilimia 85% kutokana na uboreshaji huo uliofanyika mwaka jana.

Zantel inakaribisha kila mmoja kujaribu na kufurahia huduma yake ya 4G plus inayomwezesha kupata data ukiwa mahali popote nchini Tanzania, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na huduma za kurahisisha biashara.
 Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha}- Kushoto na Mkuu wa Huduma na Upangaji Bei wa Zantel, Aneth Muga, wakionyesha bango lenye maelezo ya promosheni ya MSAKO TIME wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Kisonge mjini Zanzibar,mwishoni mwa wiki, huduma hiyo itawezesha wateja wa Zantel kutumia data kwa saa moja bure kila siku katika kipindi cha miezi mitatu.
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha}- Kushoto na Mkuu wa Huduma na Upangaji Bei wa Zantel, Aneth Muga, wakionyesha bango lenye maelezo ya promosheni ya MSAKO TIME wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Kisonge mjini Zanzibar,mwishoni mwa wiki, huduma hiyo itawezesha wateja wa Zantel kutumia data kwa saa moja bure kila siku katika kipindi cha miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad