NBAA YATOA UAMUZI DHIDI YA MAKAMPUNI MATATU YA UKAGUZI YANAYOTUHUMIWA KUKIUKA MAADILI KWA KUANDAA VITABU VIWILI VYA HESABU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 July 2019

NBAA YATOA UAMUZI DHIDI YA MAKAMPUNI MATATU YA UKAGUZI YANAYOTUHUMIWA KUKIUKA MAADILI KWA KUANDAA VITABU VIWILI VYA HESABU

KUFUATIA mazungumzo ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli na Wawakilishi wa wafanyabiashara  kutoka wilaya zote nchini Tanzania yaliyofanyika Mjini Dar Es Salaam Ijumaa tarehe 7 Juni mwaka 2019 Rais Magufuli aligusia kuwa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakiandaa vitabu viwili viwili vya hesabu (Financial Statements). Kimoja ni kwa ajili ya kuwasilishwa benki, ambacho kinaonesha matokeo makubwa na kitabu kingine kwa ajili ya kuwasilishwa Mamlaka ya mapato (TRA), ambacho kinaonesha hasara au faida ndogo na kueleza kuwa mchezo huo mchafu umekuwa ukifanywa kwa pamoja na wakaguzi (Auditors) ambao kimsingi wamesajliwa na NBAA ambayo  ni Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Rais Magufuli alisema kuwa wakaguzi/wahasibu hao hupitisha vitabu hivyo wakijua kabisa kuwa wanawasaidia wateja wao kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NBAA  CPA Profesa Isaya Jayambo Jairo amesema kufuatia  taarifa hizo NBAA kwa kushirikiana na TRA iliweza kupata majina ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu waliotuhumiwa pamoja na kampuni zilizohusika na udanganyifu huo katika kuandaa hesabu za kampuni za M / s Mek One General LTD na Mek One Industries LTD. 

Kampuni hizo za Kihasibu na Kikaguzi ni, Y.H. Malundo & Co, TEG Consultancy na MATSAB & Co na kupitia kikao cha dharura cha nne cha Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu kilichofanyika tarehe 9 Julai 2019, chini ya Mwenyekiti wake CPA. Prof.Isaya Jairo, kiliidhinisha maamuzi na adhabu mbali mbali zilizopendekezwa na Kamati ya nidhamu kama ifuatavyo, Jina la kampuni "TEG Consultancy" lifutwe (Delete) kutoka kwenye rejista ya makampuni ya Ukaguzi (Practising Firms) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa  na kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kusaini seti tatu sambamba za taarifa za kifedha ambazo hazikukaguliwa kwa madhumuni mbalimbali). 

Kampuni hiyo imeshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya kitaaluma, hivyo, kwenda kinyume na masharti ya sheria. Kwa hiyo, kampuni hii inashtakiwa chini ya Kifungu cha 17 (1) (c) & (5) kinachosomwa pamoja na Kifungu cha 21 (e), Kifungu cha 31 (1), (4) & (5) na S. 42 (c) cha Sheria kuu ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002), pamoja na Kifungu cha 16 (a) na (d), 20 a) na (b) , 27 (1) (a) na (e), Kifungu cha 29 (b) na (e) cha Kanuni za Ukaguzi za 2017 na Sehemu 210.1 210.2 na 210.3 za Kanuni za Maadili za Wahasibu na Wakaguzi Hesabu.

Pia jina la kampuni "MATSAB & CO" liondolewe) kutoka kwenye rejista ya makampuni ya Ukaguzi (Practising Firms) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kusaini taarifa za kifedha bila kukagua) kwa kuwa kampuni imeshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya Kimataifa, hivyo, kwenda kinyume na masharti ya Sheria.

 Kwa hiyo, anashitakiwa chini ya Kifungu cha S.17 (1) (c) kikisomwa pamoja na Kifungu cha 21 (e), na kifungu cha 31 (1), (4) Na (5) ya Sheria kuu, Kifungu cha 16 (a) na (d), 20 (a) na (b), 27 (1) (a) na (e), 29 (b) na (e) ya cha Kanuni za Ukaguzi, 2017 na Sehemu 210,1 210.2 na 210.3 za Kanuni za Maadili za IFAC, Kwa hiyo, kampuni imeshtakiwa chini ya Kifungu cha 21 (e), Sehemu ya 31 (1), (4) & (5) na 42 (c) ya Sheria kuu.

Vilevile  jina la kampuni "Y.H. Malundo & Company ",(kampuni ya ukaguzi), kusimamishwa kuendelea kufanya kazi za Ukaguzi  kwa kipindi cha miaka miwili (Suspension) baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Professional Misconduct) (kukagua na kusaini taarifa hesabu za kifedha bila kufuata taratibu za kisheria na miongozo ya kitaifa na kimataifa).

 Kampuni imeshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya Kitaifa na Kimataifa vya  ukaguzi wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha za M/S Mek One Industries kwa kipindi cha 2014, 2015 na 2016. Kampuni hiyo ilivunja masharti ya kifungu cha 27 (1) (b) na S. 28, Kanuni za Ukaguzi, 2017 na Sehemu ya 210.1,2 & 3 za Kanuni za Maadili ya IFAC. Hivyo Kampuni hiyo inashtakiwa  chini ya S.21 (d) ya Sheria kuu.

Jina la CPA Mazengo Kasilati (Managing Partner TEG Consultancy), kuhamishiwa kwenda kwenye orodha ya chini katika rejista (lower classification) ya (Graduate Accountant) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa  na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kusaini seti tatu za sambamba za taarifa za hesabu za kifedha ambazo hazikukaguliwa kwa madhumuni mbalimbali).

CPA Mazengo Kasilati (Mkaguzi) ameshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya kitaaluma, hivyo, kwenda kinyume na masharti ya Sheria. Kwa hiyo, anashitakiwa chini ya Kifungu cha 21 (c), na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) cha Sheria kuu, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 16 (c) na (d) cha Kanuni za Ukaguzi, na sehemu 210,1 210.2 na 210.3 ya Kanuni za Maadili za IFAC. 

Kwa hivyo, anashtakiwa chini ya Kifungu 21 (c), na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) cha Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) na CPA Mazengo Kasilati atarudisha vyeti vyote alivyopewa na NBAA vikimruhusu kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa kihasibu.

Pia imeadhimiwa kuwana la CPA Mathew J. Marapachi (Msimamizi wa M/s MATSAB na Co.), liondolewa kutoka kwenye rejista ya ACPA na yeye mwenyewe achukuliwe hatua za kisheria (mashtaka) baada ya kupata idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (Director of Public Prosecution-DPP) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa ya ukaguzi wa hesabu (Gross Professional Misconduct) (kutumia sifa ya kada ya Ukaguzi-  CPA PP) huku akijua wazi kwamba yeye hana sifa ya kufanya kazi kama 

Imeelezwa kuwa Mkaguzi wa Hesabu CPA Mathew J. Marapachi amekiuka masharti  ya   sheria na kanuni na viwango vya Kimataifa, hivyo, anashtakiwa chini ya Kifungu cha  S.17 (c), S.21 (c) cha Sheria kuu na Kifungu 14 (2), 16 (c) na (d) cha Kanuni za Ukaguzi, 2017 zikisomwa pamoja kifungu cha 27 c) kusoma pamoja na S. 42 (c) ya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

CPA Y.H. Malundo (Managing Partner- M/S Y.H. Malundo & Co.), amesimamishwa kwa muda wa miaka miwili (Suspension) baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kitaifa na Kimataifa ya ukaguzi wa hesabu (Professional Misconduct) (kukagua na kusaini taarifa za kifedha bila kufuata taratibu za kisheria na miongozo ya kitaifa na kimataifa). CPA Y.H. Malundo ameshindwa kuzingatia sheria na kanuni na viwango vya Kitaifa na Kimataifa vya  ukaguzi wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha za M /S Mek One Industries kwa kipindi cha 2014, 2015 na 2016). CPA Y.H. 

Malundo  amevunja masharti ya kifungu cha 27 (1) (b) na S. 28, cha Kanuni za Ukaguzi, 2017 na Sehemu 210.1, 2 & 3 za Kanuni za Maadili za IFAC. Kkwa hiyo, anashtakiwa chini ya kifungu cha.21 (d) ya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

Aidha bwana Mathew Kumalija (mfanyakazi wa M / s MATSAB na Co), achukuliwe hatua za kisheria (mashtaka) baada ya kupatikana na hatia ya kosa kubwa la ukiukwaji wa sheria ya Sheria kuu ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) ( kusaini taarifa za kifedha ambazo hazijakaguliwa bila kuwa na sifa za Ukaguzi).

Vile vile, afunguliwe mashtaka baada ya kupata idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (Director of Public Prosecution-DPP) kwa kosa la pili baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kutumia mitindo na majina kinyume na mahitaji ya Sheria hii.Imeelezwa kuwa  Mathew Kumalija ana sifa ya National Accountancy Diploma (NAD), sifa ambayo haitambuliwi tena na Bodi. Kwa hivyo, sio sifa ya kuajiriwa kama "Mkaguzi wa Hesabu" na pia hakuruhusiwa kusaini taarifa yoyote ya ukaguzi ya kifedha.

Hivyo, Mathew Kumalija anashtakiwa chini ya Kifungu cha 42 (c) kwa kuvunja masharti ya kifungu cha 27 b) na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) cha Sheria kuu. Kwa hivyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha 31 (1), (4) & (5)  42 (c) vya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

Pia bodi imeamuru majina ya wote waliokutwa na makosa yachapishwe kwenye vyombo vya habari (magazeti), tovuti ya NBAA na kwenye Gazeti la serikali  vilevile makampuni na watu ambao wametuhumiwa,  kusimamishwa na kushtakiwa baada ya kupata idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ( DPP) kama inavyotakiwa na S. 8 (1) ya Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002).

Pia a wamependekeza Makampuni mawili  ya M / s Mek One General LTD na Mek One Industries LTD) ambayo Ripoti ya uchunguzi ilibainisha kuwa Makampuni hayo yalivunja masharti ya vifungu cha 30 (1) (a) & (b) na kifungu cha 31 (1), (4) & (5) ikisomwa pamoja na kifungu 42 (c) cha Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi (Usajili), Sura ya 286 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia wameeleza mkakati wa kuzuia au kurekebisha hali hii isitokee tena bodi imeeleza kuwa  NBAA ipo katika hatua za kupendekeza marekebisho ya sheria iliyoiunda ili iwe na uwezo zaidi wa  kupambana na changamoto zinazojitokeza sasa ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NBAA , CPA Profesa Isaya Jayambo Jairo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Bodi hiyo mara baada ya kupata majina ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu wanaotuhumiwa pamoja na kampuni zilizohusika na udanganyifu huo katika kuandaa hesabu za kampuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad