HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 7, 2019

MAPUNDA AHAMASISHA WENYE BAA KUUNDA TIMU BORA ZITAKAZOWAKILISHA KWENYE FAINALI YA BONANZA KUBWA LA CASTLE LAGER AFRICA 5s 2019

BALOZI wa Castle Lager Africa 5s nchini Tanzania, Ivo Mapunda amewaomba wamiliki wa Baa kuunda timu bora za kiushindani zitakazowakilisha Baa zao kwenye fainali ya Bonanza kubwa litakayoshirikisha timu 32 kutoka Baa tofauti za jijini Dar es Salaam na kupata timu moja itakayowakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania mwaka huu wa 2019.
 Mapunda aliyasema hayo jana kwa Waandishi wa habari wakati akijiandaa rasmi na ziara ya kutembelea Baa 60 za jijini Dar es Salaam zilizoingia kwenye mchakato wa kiushindani kupitia promosheni zinazoendelea kwenye Baa hizo na kuwaomba wamiliki hao wajitahidi sana kuunda timu bora kwani tunatarajia kuwa na ushindani mkubwa ambao mwisho wa siku utatupatia timu moja kutoka Baa moja itakayotuwakilisha Watanzani kwenye mashindano ya Africa.
Mashindano haya yanafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza lakini ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia nhini(TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager. Hata hivyo yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika hivyo kwa fursa tuliyopewa Watanzania ya fainali za Africa kufanyika Tanzania nawasihi wamiliki wa Baa shiriki tutambue Bingwa wa fainali ya Bonanza atatuwakilisha Watanzania wote na kwa maana hiyo uundaji wa timu zetu na maandalizi kwa ujumla yanapaswa kuwa mazuri, ‘alisema Balozi wa Castle Lager Tanzania,Mapunda’.
“Mwaka jana tulishiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa ya Afrika, yaliyofanyika nchini Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia”.  
Binafsi niwapongeza sana Wadhamini wa mashindano haya Castle Lager kwa kudhamini mashindano haya ambayo yanawapa fursa wanywaji wao kushiriki michezo ambayo mwisho wa siku unatupa nafasi ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania lakini pia niwashukuru sana kwa kuniona mimi kama nastahili kuwa Balozi wa Castle Lager Africa 5s nchini Tanzania. 
 “Nafahamu Mchakato wa kupata timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo umeboreshwa zaidi mwaka huu, ambapo washiriki watapatikana kupitia katika promosheni zinazoendelea katika baa mbalimbali jijini Dar es Salaam”.
Ili kuingia 32 bora, moja ya kigezo muhimu ni kufanya mauzo mengi ambapo kutakuwa na makasha maalumu katika baa husika kwa ajili ya kukusanyia vizibo baada ya mteja kununua bia ya Castle Lager. 
Niwaombe watanzania kutumia nafasi hii, ambayo itawapa wakati mzuri wa kutimiza ndoto zao. Wakati mwingine fursa kama hizi ni nadra sana.
 Baadhi ya Wachezaji wa Baa ya Toroka Uje yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam wakishangilia mara maada ya kumaliza mchakato wa kuhesabiwa kura zao kupitia vizibo vya Bia ya Castle Lager ili kushiriki Bonanza kubwa la Castle Lager Africa 5s linalotarajiwa kufanyika Leaders hivi karibuni.
Baadhi ya Wahudumu wa Baa ya Toroka Uje wakihesabu yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam wakihesabu kura kupitia visibo vya Bia ya Castle Lager ili kushiriki Bonanza kubwa la Castle Lager Africa 5s linalotarajiwa kufanyika Leaders hivi karibuni.
 Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli akimkabidhi Balozi wa Castle Lager Africa 5s, Ivo Mapunda mpira wa miguu kuashiria uzinduzi wa mashindayo Castle Lager Africa 5s(ya wachezaji watano watano) yanayotarajiwa kufanyika Nchini mwaka huu wa 2019.
 Balozi wa Castle Lager Africa 5s, Ivo Mapunda

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad