HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 6, 2019

Waziri Mkuu aipongeza TFDA katika udhibiti

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inafanya kazi zake vizuri na kuifanya Tanzania kwa nchi Kwanza katika udhibiti wa ubora wa dawa, vifaa, Tiba, vipodozi pamoja na vitendanishi.

Waziri Mkuu Majaliwa aliyasema hayo wakati alipokwenda ziara ya kikazi katika Mamlaka hiyo amesema kuwa katika kufanya udhibiti huo waongeze kituo vya ukaguzi katika mikoa hasa katika mikoa inayopakana na nchi jirani ikiwa kwa ajili ya kulinda afya za watanzania kutokana na mwiingiliano wa dawa na vyakula nchi zilizo jirani kwa kuweza akiingia bila ukaguzi.
Amesema kuwa katika kufanya kazi za kisayansi wafanyakazi waongozwe na weledi pasipo na mwanya wa kuwepo kwa rushwa katika ukaguzi wa bidhaa mbalimbali.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa changamoto rasilimali watu atatue Waziri mwenye dhamana kwa kuomba kibali serikalini katika kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja wawekezaji wakati serikali ikiwa katika kipindi cha kuimarisha uchumi. Aidha amesema katika mnyororo wa upimaji wa bidhaa mbalimbali kusiwepo kwa Mahusiano na wataalam na mwenye bidhaa kinachotakiwa kufanyika kwa mfanyabiashara kuacha bidhaa ya kufanyiwa uchunguzi katika mapokezi na iondolewe jina la kampuni.

Amesema katika kufanya uchunguzi watalaam lazima wajiridhishe kutokana na bidhaa hizo zinaingia kwa walaji ambao lazima afya zao zilindwe. Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa TFDA inambeba katika majukwaa ya kimataifa katika umahiri wa mfumo wa udhibiti.

Amesema maagizo ya Waziri Mkuu watayasimamia katika utekelezaji ikiwa ni kuboresha huduma katika Mamlaka hiyo na kuleta matokeo katika uchumi wa viwanda. Kwa upande Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji 

Angela Kairuki amesema kuwa TFDA katika uwekezaji ni daraja na kutaka watu wenye maamuzi katika kituo vya uwekezaji ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji wanaopita (TIC).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara ya chakula ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo, Mabibo jijini Dar es salam, Machi 6, 2019. Kulia ni  Meneja wa Maabara wa TFDA, Danstan Hipolite. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika  dawa ya malaria aina ya DUO -COTECXIN,  halisi kulia na bandia kushoto zilizopimwa na kugundulika hivyo  katika  Maabara ya Mamlaka ya Chakula  na Dawa (TFDA)  wakati alipotembelea ofisi za  TFDA , Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.   Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu., kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Candita Shirima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa dawa na vyakula kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa  Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Justin Mkisi (kulia) wakati alipotembela ofisi za Mamlaka hiyo, Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki, wa nne kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tano kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Candita Shirima.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli ya mafuta ya kula yanayosubiri kupimwa wakati alipotembelea ofisi za Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mabibo jijini Dar es salaam,  Machi 6, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Justin  Mkisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) eneo la Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Candita Shirima.(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye viwanja vya Ofisi za TFDA, Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.  Wa pili kulia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad