HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 8, 2019

WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NA WATU WENGINE 14 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI PWANI KWA MAKOSA YA UHALIFU MBALIMBALI

 Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
WAHAMIAJI haramu 12 raia  kutoka Ethiopia , wamekamatwa mkoani Pwani, eneo la Mwidu porini, Chalinze kwa kosa la kutokuwa na kibali kinyume na sheria.  Aidha watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki na kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi. 

Akielezea juu ya matukio hayo, kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,ACP Wankyo Nyigesa, alisema usiku wa kuamkia march 8 ,askari polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa wahamiaji hao waliojificha kichakani eneo la Mwidu barabara ya Dar es salaam -Morogoro. 

Alieleza baada ya polisi kufika eneo hilo waliwakamata wakiwa safarini kutoka Ethiopia kuelekea Afrika ya Kusini.  :"Baada ya mahojiano ilionekana watu hao walifichwa hapo na mtu ama watu ambao bado hawajafahamika kwa lengo la kuwatafutia usafiri wa kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta ajira. "

Hata hivyo Wankyo alibainisha, afya ya wahamiaji haramu hao walikuwa wamedhoofika.  Wakati huo huo jeshi hilo linawashikilia watu nane kwa kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki. Pia watu sita wamekamatwa kwa kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kete 172.

Wankyo alielezea kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad