HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 22, 2019

TANZANIA, UGANDA ZAJADILIANA ULINZI BOMBA LA MAFUTA

Ikiwa ni muendelezo wa majadiliano mbalimbali kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP), Kamati za Ulinzi na Usalama za mradi kutoka  nchi hizo zimekutana jijini Kampala kwa lengo kujadili masuala ya usalama ya mradi huo.

Kikao kati ya pande hizo mbili kilianza tarehe 18/3/2019 na kuhitimishwa tarehe 20 mwezi huu  na Wawakilishi wa Wakuu  wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa nchi hizo mbili ambapo  kuliandaliwa Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi wa Bomba la Mafuta. 

Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi huo yanatarajiwa kusainiwa katika vikao vijavyo vya ngazi ya Mawaziri wa nchi husika.
Watendaji kutoka Tanzania na Uganda wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao chao kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
 Watendaji kutoka Tanzania na Uganda wakiwa katika kikao cha majadiliano kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
Wataalam kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha majadiliano kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad