HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 February 2019

ZERO 68 KATIKA SHULE YA SEKONDARI HASSANAL DAMJI ZAMCHEFUA RC NDIKILO

 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na matokeo ya kidato cha nne shule ya sekondari Hassanal Damji, kata ya Magomeni, Bagamoyo kwa kupata zero wanafunzi 68 na utoro uliokithiri. Kutokana na matokeo hayo ametoa miezi miwili kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, watendaji wa mitaa, kata na vitongoji kufuatilia chanzo kilichosababisha wanafunzi hao kufeli kiasi hicho wakati shule hiyo ina walimu 57 ambao wanatosha.
Akizungumza na viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule hiyo, wakati wa ziara yake mkoani hapo, Ndikilo alisema ameudhika na matokeo hayo hivyo kuna kila sababu ya kuchukua hatua mapema. Aliwaasa wanafunzi hao kuacha pia utoro na kupotelea vichakani muda wa masomo ili kuinua taaluma zao. Ndikilo aliwaambia, waache kuchezea elimu kwani ni msingi na ufunguo wa maisha yao baadae. 

"Mnakunywa uji shuleni, walimu wapo wa kutosha, kwanini wanafunzi wahaudhurii masomo??? "Namba hii sio ya kufurahisha, division one hakuna hata mmoja, division two ni wanafunzi 2,division three ni wanafunzi sita,na Four wapo 72, na zero 68 ufaulu huu lazima tuuchukulie hatua ili wanafunzi waweze kufaulu zaidi "alisisitiza Ndikilo.  Awali mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisema utoro shuleni hapo upo kwa asilimia 15 jambo ambalo sio zuri. Alisema amejipanga kuanzisha kampeni ya TOKOMEZA UTORO ili kuondoa changamoto hiyo mashuleni. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad