HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 14 January 2019

Wananchi kata ya Kala wamlilia RC baada ya kukosa mawasiliano ya simu na radio

Wananchi wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya kata

Kilio hicho kimetolewa wakati wa kusoma risala ya maendeleo ya kata na msoma risala Felix kapoze alipokuwa akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo kwa muda mrefu jambo linalokwamisha utendaji kazi pamoja na kufanya mawasiliano kuwa magumu.

“Changamoto nyingine kubwa ilipo hapa Kijijini kutokuwapo kwa mtandao wa simu, hii inapelekeana kukwama kwa taarifa nyingi hasa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hivyo tunaiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa itusaidie kupatikana kwa mtandao wa simu ili kurahisisha mawasiliano,” Alifafanua.

Halikadhalika jambo hilo liliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Desderius Mipata wakati akielezea changamoto hiyo na hatua alizochukua kuhakikisha kuwa mawasiliano hayo yanapatinaka na hatimae kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za maendeleo katika kata hiyo.

“Hawa wananchi ni pekee ambao hawazungumzi na wenzao katika taifa na katika jimbo, juhudi nilizozifanya kama kiongozi wa jimbo ni kuitaka wizara ihakikishe kwamba tunapata mtandao, tunashukuru mungu wametusikiliza na sasa wanajenga minara miwili katika Kijiji cha kilambo cha mkolechi na Kijiji cha Kala, wanasema Kala itazungumza wantuambia katika kipindi kisichozidi miezi miwili,” Alibainisha.

Nae Wangabo aliwahakikishia wananchi wa kata hiyo kuwa mawasiliano yataimarishwa “Tutaimarisha hayo mawasiliano na juzi nilikuwa naongea na waziri wa ujenzi alikuja pale ofisini na tuliongea swala hili la minara ya mawasiliano, uzuri wameshaanza kufanyia kazi, kwahiyo tutaongeza nguvu kule ili mitandao ya mawasiliano ifanye kazi n ahata radio nkasi iweze kuwafikia huku,” Alisema.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mpasa, Kata ya Kala mwambao wa ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpasa, Kata ya Kala mwambao wa ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akiongea na mlemavu wa miguu aliyesimamisha msafara wa Mkuu huyo ili kumsalimia katika kijiji cha mlambo kilichopo katikati ya Kijiji cha Mpasa na Kingombe vilivyotengwa kwa kilometa 34 na hakuna mawasiliano ya simu wala radio katika Kata ya Kala  Wilaya ya Nkasi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akisalimiana na mlemavu wa miguu aliyesimamisha msafara wa Mkuu huyo ili kumsalimia katika kijiji cha mlambo kilichopo katikati ya Kijiji cha Mpasa na Kingombe  Kata ya Kala  Wilaya ya Nkasi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad