HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 14, 2019

GULAMALI AZIDI KUIMARISHA SEKTA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIKA utekelezaji ahadi kwa wananchi kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mbunge wa jimbo la Manonga, Seif Gulamali ameendelea na uboreshaji wa miundombinu hususani katika sekta ya elimu na afya ili kuhakikisha wananchi jimboni humo wanakuwa na afya bora na wanapata elimu yenye tija.

Akizungumza na  blogu ya jamii Gulamali amesema, suala la elimu kwa sasa hali ni shwari kabisa hasa kwa wanafunzi wapya anaoanza kidato cha kwanza kwani  wanafunzi wamekuwa  wengi kuliko siku za nyuma na wamejipanga vyema katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimo bora na bure na mkakati uliopo sasa ni kuendelea kujenga Shule mpya na kuongeza madarasa katika Shule zilizopo, amesema kuwa  wanatarajia kuongeza shule mpya  katika  Kata za Kitangiri, Ugaka, Igoweko, Mwamala, na Tambarale ambako  Wananchi wameonesha ari ya Kuchangia Ujenzi na yeye kama Mbunge atawaunga mkono kwa kuhakikisha Shule zote zinakamilika kwa Wakati.

Amesema kuwa  shule mpya ya Ibologero iliyoanza kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwaka huu wamepewa jumla ya shilingi milioni 4.5 kwa ajili ya uendeshaji na shule ya Kitangiri imeshapokea shilingi milioni 3.5 kwa mwaka huu wakiwa wanapokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza.

Aidha amesema kuwa pesa zimetolewa kwa ajili ukarabati wa madarasa na vyumba vya madarasa katika vijiji vya Mpogolo, Ncheli, Moyofuko, Kitangiri pamoja na Mondo.

Pia huduma za umeme na maabara  pamoja na ofisi na nyumba za walimu katika kijiji cha Ngulu unaendelea na hiyo ni sambamba na   ukarabati wa bweni katika sekondari ya Ziba ambapo jumla ya shilingi milioni saba zimetolewa.

Aidha Gulamali  amesema kuwa  Zahanati ya Nkinga imeshapata huduma ya maji na hiyo ni baada ya Mbunge  na waganga wa tiba asili kuungana katika kuchangia uboreshwaji wa huduma ya maji pia amesema kuwa katika kijiji cha Ugaka ambako Zahanati inajengwa tayari wamepatiwa mifuko 50 ya saruji na shilingi milioni 9.

Gulamali amesema kuwa  zaidi ya shilingi milioni 52 za mfuko wa jimbo zimetolewa kutokana na maombi aliyopokea kutoka kwenye kamati  husika za ujenzi na amesema kuwa ana imani kuwa viongozi  wa vijiji watasimamia kwa ufanisi na mapema mwaka huu atajiridhisha kupitia ziara yake atakayoanza hivi karibuni.

Mbunge wa jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Gulamali

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad