HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 14 January 2019

CHUO CHA IFM WAONGEZA KOZI YA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA HIFADHI YA JAMII


Na Khadija Seif, Globu ya jamii
CHUO cha usimamizi wa fedha  nchini (IFM) kimeanzisha kozi ya shahada ya uzamili katika hifadhi ya jamii. Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea rasimu hiyo Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Emmanuel Mnzava amewapongeza  wawakilishi kutoka vyuo vishiriki Saba Muco, IFM, Ustawi wa Jamii, Tengeru, Udsm na kukiteua Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuwa cha kwanza katika kuanzisha mtaala huo wa shahada ya Hifadhi ya Jamii chuoni hapo ikiwa ni shahada ya pili.

 Mnzava amefafanua kuwa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) kipo kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuboresha elimu na kuelekea uchumi wa viwanda chuo hicho kitaweza kuzalisha wafanyakazi watakaohitaji kulindwa hasa kwenye kipengele cha bima na mafao .

Amewaomba vyuo vishiriki kuchukua wakufunzi wabobezi watakaojiunga na mtaala huo ili kuleta wataalam wenye kuleta tija na maslahi kwenye nchi kwa ujumla ambapo mtaala umezingatia mahitaji na hivyo wasomi kupewa watapewa kipaumbele na ili kuongeza ujuzi zaidi .

"Changamoto zilikua ni nyingi katika utayarishaji wa mtaala huu lakini kamati iliweza kufanya kazi nzuri na Mia ambapo leo tumeweza kupata mawazo Bora katika kuelekea uchumi wa viwanda naamini tutaweza kuzalisha wataalam wengi wenye weledi na waliotukuka"alisema mnzava

Kwa upande wake Mkuu wa kitivo katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) Baghayo Saqware amesema Muungano huo wa vyuo vishiriki Saba umeunda mtaala ambao utaleta tija kwa wataalam hususani kwenye ngazi ya bima ,sera na kiutendaji.

Aidha, Saqware amesema mtaala huo utaweza kukidhi mahitaji ya soko hasa katika hifadhi za jamii na  kuleta tija na manufaa kwa kuwepo kwa wataalam wengi. "Napendekeza kwa upande wa (NACTE)kupitisha mtaala huo mapema ili mafunzo yaweze kuanza rasmi "alisema Saqware.

Muwakilishi kutoka chuo kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) Nassor Nassor amepongeza chuo cha usimamizi wa fedha( IFM) kwa kuuona mchango wa vyuo vishiriki katika kuwasilisha mawazo na maoni na hatimae kufanyia kazi ipasavyo na kuletwa rasmi kwa rasmu ya mtaala huo wa shahada ya uzamili katika hifadhi ya jamii.

"Naamin mapendekezo mengine yataweza kufanyiwa kazi ili kuleta chachu ya Maendeleo katika sekta ya hizo hasa kukuza taaluma nchini "alisema Nassor.
Makamu Mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) Dkt. Emmanuel Mnzava na Mkuu wa kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii cha chuo hicho Kidadi Mashawishi baada ya kupokea rasimu hiyo ya mtaala wa shahada ya uzamili katika hifadhi ya jamii jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Emmanuel Mnzava akipokea rasmu ya mtaala mpya wa kozi ya shahada ya uzamili katika Hifadhi ya Jamii kutoka kwa mwakilishi wa vyuo vishiriki Saba leo jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad