HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 20 January 2019

AFISA ELIMU ASIMAMISHWA KAZI ARUSHA

Na Vero Ignatus, Arusha. 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemsimamisha kazi Ofisa elimu wa mkoa huo Gift Kyando kwa madai ya kuzuia wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza huku akilazimisha kila darasa kuwa na wanafunzi 40 tu.  Pia anadaiwa kusababisaha wanafunzi hao kukosa nafasi za masomo kwa kukataa kusajiliwa kwa shule mbili mpya za Oldonyowasi na Losikito kwa madai ya kukoda mahabara.

Gambo amesema kitendo hicho ni cha kukwamisha juhudi za serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwa uamuzi aliouchukua Ofisa huyo haukumuhusisha kiongozi yeyote yule wa serikali ngazi ya wilaya au mkoa. Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Dk. Wilson Mahera amesema kitendo hicho alichokifanya  ofisa huyo kiliwachanganya na kusababisha ugomvi kati yao na   wazazi wa wanafunzi hao 

Amesema ofisa huyo angesababisha wanafunzi 6,819 kukosa elimu  wakati yapo madarasa ambayo yaliachwa na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne ambayo yangeweza kutumiwa na wanafunzi hao
'' Madarasa yaliyopo yangeweza kuchukua wanafunzi  kwa kipindi kifupi wapatao 55 kwa darasa moja '' alisema Mahera

Dkt. Mahera amesema kuhusu mapokezi  wanafunzi kati ya shule 4239 wameshapokelewa katika shule 28 za halmashauri ya Arusha wakiwemo  wavulana 1,853 na wasichana 2,386 ambao ni sawa na asilimia 62 huku waliobakia wakiendelea kuripoti na wengine wakichukua fomu za kujiunga. 

Kwa upande wake Mwenyakiti wa CCM mkoa Loata Sanare amesema alichokiona ni hujuma za waziwazi kwa ofisa huyo  dhidi ya serikali na kutaka kuzuia wanafunzi wasianze masomo. Sanare anasema alianza kupokea simu za malalamiko kutoka kwa wazazi wawanafunzi hao na alipompigia ofisa elimu huyo alimjibu majibu ambayo hayakumridhisha ndipo alipoamua kuwasikiana na mkuu wa mkoa. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad