SHAMTE AMEWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA ZINAZOJITOKEZA HAPA NCHINI KUENDELEZA BIASHARA ZAO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

SHAMTE AMEWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA ZINAZOJITOKEZA HAPA NCHINI KUENDELEZA BIASHARA ZAO

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Salum Shamte amewataka vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi kutumia fursa inayotolewa na Shirika la Angel  Investors (Wawekezaji Malaika) ambalo limekuja nchini kuwafikia Watanzania kwa kutoa mitaji kwa Wafanyabiashara wadogo ili kupiga hatua.

Shamte ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi maalumu wa ufunguzi wa Ofisi ya Taasisi inayohudumia Vijana ambao ni wavumbuzi, wabunifu wanaoanza biashara ambapo watasaidiwa na Taasisi ya World  Business Angel Investment  Forum (WBAF) ambayo limejikita kupeleka huduma za kifedha  kwa Vijana hao. Aidha Shamte amesema kuwa asilimia  kubwa ya vijana hapa nchini wana ukosefu wa ajira pamoja na kupata mtaji wa kujiendeleza  katika biashara.

Mkurugenzi Mkazi wa Angel Investors  Tanzania (Wawekezaji Malaika), Sabetha Mwambenja amesema kuwa tayari wamesha fanya mazungunzo na Sekta ya Umma na Binafsi ikiwamo Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Mtakatifu Joseph, Chuo Kikuu cha Tumaini, VETA, COSTECH, Taasisi yaTeknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Kilimo cha Sokoine, (SUA), Chuo cha All Makhoum cha Mbezi Beach na  Hatamizi za Tehama (Incubators). 

Mwambenja amesema kuwa kwa kuanzia Taasisi ya WBAF imeshafungua Milango ya  kuwawezesha walengwa kutumia maombi kwa Angel Investors Tanzania waweze kuunganishwa na Taasisi hiyo ambayo kupitia kamati yake ya uwekezaji itakayopokea maombi ya maandiko ya miradi husika na kuyachuja. 

"Mpaka sasa Vijana zaidi ya 500  wameshaunganishwa kupitia kiunganishi (Link) ambapo watachujwa na kufika 66 watakaoenda kufanyiwa uwasilishaji katika Mkutano wa mwaka wa siku tatu wa Angel Investors wa Dunia unaotarajiwa kufanyika Makao Makuu yake Instabul nchini Uturuki kuanzia February 18 mpaka 20 mwakani mwakani", amesema Mwambenja. 

Hata hivyo, Kijana Mvumbuzi Robert Aseyi ambaye amebuni Mfumo wa Kieletroniki inayofanya kazi yoyote ukiwa mbali kuendesha vitu vyako kwa kutumia simu ya mkononi aina ya Smartphone ameelezea  changamoto alizokumbana nazo mpaka kukamilisha ubunifu huo, ikiwemo vifaa kuchukua muda mrefu kufika.

Vile vile, Aseyi amesema  kuwa bado hajafikia malengo yake vizuri ili iwe na muonekano wa kibiashara ipate kuuzika licha ya kujibana katika matumizi yake ya kifedha, anaamini WBAF itaweza kuwasidia  kumunganisha na wawekezaji kupata mtaji wa kujiendeleza malengo yake.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania Salum Shamte akisistiza suala la Vijana waso kutumia fursa inayotolewa na Taasisi ya World Business  Angels Investment  Forum (WBAF)  lililojikita kutoa huduma za kifedha kwa Vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi wanaoanza biashara  kupiga hatua na kuwa wafanyabiashara wakubwa, leo katika ufunguzi wa ofisi ya taasisi ya WBAF Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi wa Angel Investors  Tanzania Dkt Sabetha Mwambenja akifafanua ujio wa taasisi hiyo wakati wa ufunguzi huo wa ofisi ya WBAF hapa nchini, kuwa ni kutaka kuinua Vijana wasomi katika suala zima la kujiajiri kwa kuwawezesha namna ya kupata mtaji ili kujikwamua kiuchumi  wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Biashara na Maendeleo nchini Ghana Ibrahim Awal  ambaye pia ni mkulima amehudhuri ufunguzi huo wa ofisi ya WBAF hapa nchini wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam..
Mwenyekiti Taasisi ya World  Business  Angels Investment  Forum (WBAF), Baybars Altuntas akizungumzia taasisi hiyo kuwa inafanya kazi zake katika nchi zaidi ya 66 hapa duniani wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam..
  Mkurugenzi Mkazi  Angel Investors  Tanzania Dkt Sabetha Mwambenja (kushoto) na Mwenyekiti WBAF  Baybars Altuntas (kulia) wakionyesha mafaili kuashiria ufunguzi wa ofisi ya WBAF hapa nchini umeshakamilika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad