HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 29, 2018

AZAM YAJIZATITI KUTETEA UBINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Azam FC, imepangwa kundi moja na Yanga kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2019 inayotarajia kufanyika kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani Visiwani Zanzibar.

Azam FC ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo ikibeba mara mbili mfululizo, mbali na kupangwa Kundi B pamoja na Yanga, kundi hilo pia lina timu nyingine za Malindi, KVZ na Jamhuri ya Pemba.

Mabingwa hao wataanza kampeni ya kuanza kutetea taji kwa kupambana na Jamhuri, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Januari 2 mwaka huu saa 2.15 usiku kabla ya Januari 5, kukipiga na Yanga.

Aidha, Azam FC itamaliza hatua ya makundi kwa mechi mbili dhidi ya KVZ (Januari 7, 10.15 jioni) na kufunga dimba Januari 9 kwa kumenyana na Malindi saa 2.15 usiku.

Baada ya hapo, Azam FC itasubiria hatua ya nusu fainali itakayohusisha timu mbili zitakazoshika nafasi mbili za juu kwa kuwa na pointi mbili kwenye makundi yote mawili na washindi wa mechi hizo mbili wataingia fainali itakayopigwa kwenye Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Kundi A la michuano hiyo linahusisha timu za Simba, KMKM, Mlandege na Chipukizi.

Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, imesema kuwa zawadi kwa mshindi wa kwanza itaongezwa kutoka shilingi milioni 10 hadi kufikia shilingi milioni 15 ikiwa ni pamoja na medali za dhahabu pamoja na kombe.

Mshindi wa pili naye naye atapata shilingi milioni 10 badala ya milion 5 iliyokuwa ikitolewa awali, na medali za fedha.

Katika hatua nyingine itakuwa imeandika rekodi ya kuwa timu pekee iliyofanya hivyo, na timu pekee kulitwaa mara nyingi taji hilo ikifanya hivyo mara tano na itakuwa imeiacha Simba iliyolitwaa mara nne.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad