Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wamezindua chapa mpya kwa bidhaa yao ya OTT (Application), itakayokuwa ikijulikana kwa jina la StarTimes ON. Bidhaa hiyo inakuwa ya kwanza kabisa barani Africa kutoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa teknolojia ya kisasa zaidi ili kuongeza burudani na utazamaji mzuri zaidi.
Uzinduzi huo wa StarTimes ON umekuja baada ya App ya awali (StarTimes App) kufanyiwa maboresho makubwa na kuwa StarTimes ON. StarTimes ON imekuja na Luninga Mubashara, VOD (Video on Demand) pamoja na video fupi ambazo zitakuwa na maudhui mbali mbali kuanzia Habari, michezo, tamthiliya, muziki, burudani, makala, vipindi vya watoto pamoja vipindi vya dini.
“StarTimes ON inamsaidia mtumiaji kuokoa hadi asilimia 40 ya data (bando) wakati anapotumia, tofauti na matumizi ya kawaida ya kuangalia video mtandaoni. Naweza kusema StarTimes ON ni mapinduzi katika upatikanaji wa maudhui mtandaoni.” Mussa Shaaban Lindo, StarTimes ON App Operator.
“Kwa sasa, kuna zaidi ya chaneli 150 ambazo zinapatikana kwa ligha zaidi ya 10 kwenye StarTimes ON huku chaneli 140 kati ya hizo zikiwa ni chaneli za buree. Miongoni mwa chaneli hizo ni ST Swahili ambayo kwa sasa ina vipindi Bomba kabisa kama shindano la Bongo Star Search ambalo linaendelea na kuna video kibao za waashiriki wote unaweza kuziangalia muda wowote mahali popote ili mradi tu uwe na intaneti inayofanya kazi”. Bw David Malisa, Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes.
Pia StarTimes ON ina chaneli zaidi ya 40 za StarTimes, huku watumiaji wakiwa na uwezo wa kuona maudhui mapya kila siku.Pamoja na hayo yote, kupitia StarTimes ON watumiaji wanaweza kuwapigia kura washiriki wawapendao katika shindano la Bongo Star Search, wanaweza kutazama Show mbali mbali za washiriki wa BSS na kuwatumia maua majaji wa BSS, StarTimes ON ni App ya kwanza Tanzania yenye aina hiii ya utumiaji.
Kupitia StarTimes ON watumiaji wanaweza kutazama michezo mbalimbali kama vile Ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, Ligi ya Ufaransa (Ligue 1), ligi ya UEFA EUROPA inayoendelea Alhamisi wiki hii. Kwa sasa Mechi za Bundesliga na Ligue 1 zinaonekana moja kwa moja pia kutazama marudio ya mechi hizo muda wowote na sehemu yoyote.
No comments:
Post a Comment