HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 10, 2018

WAZIRI NDALICHAKO: SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENZI YALE YOTE ALIYOISHI MWALIMU NYERERE


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema falsafa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zimepata msukumo wa hali ya juu katika serikali ya awamu ya tano kwa kuwataka watanzania kufanya kazi kwa bidii.

Prof Ndalichako amesema hayo leo Mapema Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kongamano la Siku mbili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni  lililokuwa na Mada inayosema  'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa la Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'

"Mwalimu Nyerere alisisitiza kufanya kazi kwa bidii na udalifu na kusimamia msingi wa uzalendo kwani Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dk. John Magufuli ameweza kusimamia neno la hapa kazi tu ambalo ni moja ya Falsafa ya Mwalimu Nyerere iliyosema kuwa kufanya kazi kwa bidii , Kazi ni Uhai na Kazi ni Utu hivyo tunapaswa kujiuliza hii falsafa ina umuhimu gani katika kufanikisha kuelekea nchi ya uchumi wa Viwanda"

Prof Ndalichako amesema kuwa kuna mambo mengi yanafanywa na Serikali ya awamu ya tano  ambayo yalianzishwa na Baba wa Taifa wa Mwalimu Nyerere hivyo hii falsafa iweze kuangaliwa ni namna gani itaweza kuleta mchango wa Maendeleo ya Viwanda katika Taifa hili kwani mada iliyochaguliwa ina akisi msisitizo wa serikali yetu.

Alisema kuwa nia ya Serikali hii ni kuendeleza miradi Mikubwa ambayo ndio Msingi wa kufikia Maendeleo ya Haraka kama ujenzi wa mardi mkubwa wa umeme wa Stiglizers  Gorge ambao utasaidia kuzalisha umeme mkubwa katika nchi hii  ambayo ni Nishati Muhimu

Alimaliza kwa kuwataka watanzania kuunga mkono Juhudi za Rais wetu ambaye amekuwa kipaumbele katika kusimamia rasilimali za Taifa hili tuweze kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati hivyo waswahili usema 'penye nia pana njia'
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamno la Kumbukumbu la kuenzi kazi zilizofanywa na Mwalimu Nyerere lilolikuwa linahusu 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa la Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,Mashavu Fakih akizungumza kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi
 Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Shadrack Mwakalila akizungumza na watu waliofika katika kongamno hilo.
 Baadhi ya Viongozi Wastaafu walioshiriki katika Kongamano hilo la 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dr .Bashiru Ally Bashiru akifatilia Mdahalo wa 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda' uliofanyika katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Magogoni Dar es Salaam
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad