HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 14 October 2018

ARUMERU YAMUENZI MWALIMU NYERERE KWA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA

 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro leo amewaongoza waumini wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Meru Usharika wa Maruvango katika Mtaa wa Maruvango katika ibada ya Kuadhimisha miaka 19 ya Kifo Cha Baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo katika Ibada hiyo pia Mhe Muro aliendesha Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Maruvango na kufanikiwa Kuchangisha Jumla ya Shilingi Milioni 28,331,500 Fedha zilizopatikana Kutokana na Ubunifu na Hamasa  ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambae alilazimika kufanya kazi ya Ziada ya kuhamasisha wananchi na kufikia Malengo.
 Katika Ibada Hiyo Dc Muro amewataka wananchi wa Arumeru kumuenzi Mwalimu Kwa kuzingatia misingi ya Umoja na Amani ya Nchi, Dc Muro amesema katika Uhai wake Mwalimu Nyerere alipinga vitendo vya Rushwa na Ufisadi, uonevu, ukandamizaji wa Haki za Msingi za wananchi haswa Kina Mama na watoto , Mwalimu Nyerere alisisitiza matumizi bora ya Ardhi ambapo Kwa wilaya ya Arumeru Bado Migogoro ya Ardhi imeendelea kuwa changamoto hatua ambayo imemlazimu Dc Muro kuomba viongozi wa Dini kuendelea kuiombea Wilaya ya Arumeru kuepukana na Migogoro ya Ardhi.
Katika Mahubiri yake , Mchungaji wa Usharika Mchg Aminiel Mwenda amesema Kanisa litaendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere Kwa kuwasisitiza wananchi kuacha Vitendo viovu vya rushwa, ufisadi, dhuluma na Chuki, ambapo amesema Katika utawala wa awamu ya tano chini ya  Rais Dkt. John Pombe Magufuli umeanza kurudisha Mwelekeo na Matendo ya utawala wa Mwalimu Nyerere Kwa kukomesha vitendo vya Rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi ambapo amemuomba Mhe Magufuli kuendelea na jitahada zake za kuitengeneza Tanzania Mpya ya viwanda na yenye uchumi wa kati.

Katika Harambee hiyo Dc Muro alialika marafiki, ndugu na Jamaa wanaoishi Arumeru na kutoka katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Arusha akiwemo Bw Richard Kashaija kutoka Dar es Salaam ambae ameoa Arumeru.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad