HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 3, 2018

MTENDAJI MKUU TFS ATOA NENO KWA WASHIRIKI MISS TANZANIA 2018

*Awataka wawe mabalozi kuhimiza uhifadhi wa misitu,utalii wa ndani
 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAREMBO wa Shindano la Miss Tanzania 2018 wametajwa kuwa mabalozi wazuri wa Vivutio vya Utalii nchini ikiwemo Rasilimali za Misitu na Nyuki pamoja na Maporoko.

Akizungumza na Warembo hao jijini Dar es Salaam wakati anawaaga wakielekea katika hifadhi ya Amani mkoani Tanga, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amewataka walimbwende hao kutumia weledi, uwezo Kitaaluma na nafasi katika jamii kusaidia uhifadhi wa misitu.

Prof. Silayo amewataka warembo hao kutangaza Misitu hiyo mazuri yake ili iweze kutumika kutoa huduma za kiutalii na kuonesha thamani yake iliyosimama.

Amesema uhifadhi wa misitu unaifaida nyingi na moja ya faida misitu ni cha chanzo uhifadhi wa maji na kuongeza pamoja na hewa safi.

Amesema kuwa TFS itatumia sehemu ya washiriki hao wa Miss Tanzania mwaka huu kwa ajili ya kuwa malozi ambao watashiriki kikamilifu kuhimiza uhifadhi misitu.

Amefafanua watawajengea uwezo katika kuhakikisha wanaifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na zaidi kuna maeneo mengi ya misitu ambayo imehifadhiwa ambayo inahitaji mabalozi wa kutangazwa.

"TFS pamoja na wadau wengine wakiwamo wa utalii nchini ambao wapo Wizara ya Maliasili na Utalii tumeamua kushirikiana na  ya Miss Tanzania kuhakikisha washiriki watano wa Miss Tanzania tunawatumia kuutangaza vivutio vya utalii na uhifadhi misitu,"amefafanua Profesa Silayo.

Amesema katika kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri warembo hao watatembelea baadhi ua misitu iliyohifadhiwa ukiwamo hiyo hifadhi ya msitu Amani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi amesema kuwa lengo la ushiriki wa taasisi za utalii katika Shindano hilo la Ulimbwende ni kukuza utalii wa ndani.

Mwanukuzi ameeleza kuwa taasisi za utalii zimeunga mkono kuhakikisha Utalii unatangazwa na hivyo washiriki watano kati ya 20 waliopo kwenye shindano hilo watapata fursa ya kuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi wa misitu.


Mwanukuzi amesema kutakuwa na mabalozi watano katika Shindano hilo la Miss Tanzania 2018 wamegawanyika katika sehemu tano.

Ametaja kutakuwa na Miss Domestic Tourism, Miss Ruaha, Balozi TANAPA), Miss Ngorongoro, Miss Seleu(Tanzania World Life Authority) na  Miss Equal Tourism chini ya Forest Services.

Kuhusu shindano la Miss Tanzania ,Mwanakuzi amesema wameshusha bei ya kiingilio ili kutoa fursa ya watanzania wengi kushuhudia.

Ametaja viingilio hivyo ni kwamba  VVIP 70,000, VIP 50,000 na kawaida 30,000.

Amesema lengo la mashindano hayo si kupata faida bali kuhakikisha jukwaa hilo linatoa fursa kwa watoto wa kike kuwa daraja katika kutimiza ndoto zao kwani anaamini baada ya mashindano hayo watashiriki kufanya kazi za kijamii kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
 Washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Msitu Amani mkoani Tanga.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 baada ya kuzungumza nao kuhusu umuhimu wa warembo hao kuutangaza uhifadhi wa misitu na utalii nchini
 Muandaji wa Mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2018 Basila ambaye pia amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998 akiwa na Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Sontos Silayo wakati wakizungumza na washiriki wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(wa pili kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2018 kutoka Kanda ya Ziwa ambao pia ni mabalozi wa kuyatangaza  maporomoko ya Karambo
 Washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 wakiwaaga viongozi kutoka taasisi mbalimbali za utalii pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kabla ya kuanza kwasafari ya kuelekea katika Hifadhi ya Amani mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad