
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji
wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount
katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika jijini Dar es
salaam leo. Kulia ni
Mkurugenzi wa CRDB Micro Finance, Sebastian Masaki pamoja na Msimamizi
wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Mohamed.
Benki ya CRDB leo imezindua kampeni maalumu
ya utumiaji wa huduma zake ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount
ambayo inawapa wateja wa benki pamoja na Watanzania kwa ujumla nafasi kujishindia fedha
taslimu zaidi ya shilingi milioni 200.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama “Shinda na SimAccount”,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema Benki ya CRDB imeamua
kuanzisha kampeni hiyo ili kuwahamasisha watanzania kujiunga na kutumia mfumo wa SimAccount
ambao ni rahisi, nafuu na haraka.
Katika kampeni hii ya “Shinda na SimAccount”, wateja waliojiunga na kutumia huduma mbalimbali
zinazopatikana ndani ya mfumo wa SimAccount watajishindia zawadi za fedha ambapo kila siku
washindi 24 watakuwa wanapatikana, pamoja na washindi 12 wa wiki, washindi wa 3 wa mwezi na
mshindi wa kampeni nzima "Jackpot Winner" atakaye patikana mwishoni mwa kampeni na
kujishindia zawadi ya shilingi milioni ishirini.
"Unachotakiwa kufanya katika kampeni hii ni kujiunga na SimAccount kwa kupiga *150*62#,
pamoja na kuitumia kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kuweka na kutoa pesa kwenye
matawi ya Benki ya CRDB, Mawakala wetu wa SimAccount na FahariHuduma Wakala” alifafanua
Mkurugenzi huyo Mtendaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kushoto)
akibonyeza kitufe kwenye luninga kuashiria uzinduzi wa kampeni maalumu
ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo
kama SimAccount iliyo chini ya Kampuni tanzu ya Benki (CRDB Micro Finance) katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”,
iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa
Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi
wa CRDB MicroFinance, Sebastian Masaki pamoja na Msimamizi wa Michezo ya
Kubahatisha nchini, Humud Mohamed.
SimAccount ni mfumo maalum wa utoaji huduma unaowezesha watanzania kujisajili na kufungua
akaunti kupitia simu za mkononi. Mfumo huu ulizinduliwa rasmi tarehe 26 Agosti Mwaka jana na
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mama Samia Suluhu Hassan, ukiwa na
lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi na usalama kwa watanzania wengi
hata wale wasio na akaunti za benki kupitia simu zao za mikononi “Simu Yako, Akaunti Yako”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa kampeni
maalumu ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi
ijulikanayo kama SimAccount katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”,
iliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
Akielezea baadhi ya faida za kujiunga na mfumo wa SimAccount kwa wateja, Dkt Charles Kimei
alisema mfumo huu unawapa fursa wateja;
- kufungua na kusimamia akaunti za vikundi mbalimbali ikiwemo vya kusaidiana, VICOBA, Harambee, harusi n.k.
- uwezo kufungua akaunti mbalimbali kwa ajili ya kuweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali mteja aliyojiwekea.
- mfumo huu mteja ataweza kulipia manunuzi ya bidhaa kwenye maduka ya kawaida yanayopokea malipo kwa SimAccount kwa Mangi, Saluni, Mama Ntilie n.k

Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) akishuhudia zoezi
la upigaji simu kwa washindo wa promosheni ya “Shinda na SimAccount”.
Dkt. Kimei alisema uzinduzi wa kampeni hiyo ya “Shinda na SimAccount” unaleta chachu kwa
watumiaji wa SimAccount kuendelea kufurahia huduma hizo huku wakijiweka katika nafasi nzuri ya
kijishindia zawadi kubwa ya magari.
Akimalizia hotuba yake Dkt. Kimei alitoa rai kwa wateja na watanzania wote kwa ujumla kujiunga na
SimAccount kwani ni mfumo madhubuti wa kibenki utakaowawezesha kufanya miamala yao kwa
urahisi zaidi, pamoja na kijishindia zawadi mbalimbali katika kipindi cha miezi minne ya kampeni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa
No comments:
Post a Comment