HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 4 September 2018

BUNDESLIGA YAWA MOTO, LIVE KWA KISWAHILI KUPITIA STARTIMES

MSIMU wa Bundesliga kwa Kiswazi umeanza rasmi ikiwa ligi yenye kasi na maarufu kwa kuzalisha wachezaji Vijana wenye vipaji. Kwa mara nyingine Kampuni ya Star Media   imewaletea wateja wao msimu mpya wa Bundesliga wakiwa na  matarajio  makubwa sana kwa timu zote hivyo wateja wao  watafurahia.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja masoko wa Startimes David Malisa kuhusiana  kurejea kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga msimu wa 2018/19 amesema kuwa
ligi hiyo ya Ujerumani ni miongoni mwa ligi kubwa na bora kabisa barani ulaya, ikiwa na wachezaji mahiri kama mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Lewandowski, Marco Reus, mjamaica Leon Bailey na wengine wengi. Katika msimu huu wa 2018/19 StarTimes imezidi kuinogesha Bundesliga kwani itakuwa ikitangazwa kwa lugha ya. Kiswahili.

“Ikumbukwe kwamba StarTimes pekee ndio tunaonyesha ligi ya Bundesliga na sasa burudani inaongezeka maradufu kwa sababu mechi zitatangazwa kwa lugha yetu ya nyumbani yaani Kiswahili, na wachambuzi makini kabisa wenye weledi katika soka la ulaya. Pia mechi zote zitakuwa zikipatikana kwa kiwango cha HD kwenye chaneli zetu za Michezo”. Ameeleza Malisa. David Malisa, Meneja Masoko.

Aidha Malisa amesema kuwa mbali na ligi ya Bundesliga, StarTimes watarusha ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 na wapenzi wa soka wajiandae kushuhudia kandanda safi kutoka kwa  Neymar na kinda machachari Kylian Mbappe.

Kwa upande wake Meneja Maudhui wa StarTimes Bi. Zamaradi Nzowa alimewatambulisha mastaa kadhaa ambao watafanya nao kazi katika kuhakikisha taarifa zinafika kwa wakati kwa wateja ambao muda mwingi wanakuwa katika mitandao ya kijamii. Amewatambulisha Madee, Dogo Janja, na  Mkali wenu kama mabalozi.

"Tunataka kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali” ameeleza Bi. Zamaradi.

Meneja masoko wa Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kurejea kwa msimu wa pili wa kutazama kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga 2018/19 kupitia king'amuzi cha Startimes. kulia ni Meneja Maudhui wa StarTimes,  Zamaradi Nzowa.
Meneja Maudhui wa StarTimes,  Zamaradi Nzowa akizungumza na waandihsi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kutazama kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga 2018/19  katika ofisi za kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga Abduli – Aziz Abubakari Chende "Dogo janja" akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na ligi hiyo. Kushoto ni Meneja masoko wa Startimes David Malisa.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad