HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 2, 2018

WADAU WA AFYA WAJITOKEZA KUCHANGIA VIFAA CHALINZE

Na Shushu Joel, Chalinze
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania health promation support (THPS) inayofanyakazi kwenye mikoa yote nchini Tanzania, imekabidhi 
vifaa vyenye thamani ya sh. Mil. 48.4 kwa ajili ya kusaidia baadhi ya mahitaji katika  Kituo cha afya cha Msoga. 

Hayo yamebainishwa na Dkt. Sisty Moshi wakati alipokuwa akisoma taarifa yake mbele ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze  Ridhiwani Kikwete katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwenye kituo hicho.

Taarifa hiyo imesema kwamba taasisi hiyo kupitia mradi wa kusaidia kuzuia maambukizi mapya ya VVU, kutoa huduma , tiba na msaada wa kisaikolojia kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani inafanyakazi katika mikoa ya Kigoma, Pwani na Visiwa vya Zanzibar.

Aliongeza kuwa ufadhili huo unatokana na makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani kufuatana na malengo ya Kitaifa na kuboresha miundombinu ya sekta ya afya, mhuku akisema kwamba kwa Mkoa wa Pwani wamekabidhi vifaa vyenye thamani ya sh. Mil. 761.5 kwa mwaka wa 2016 na 2018.

"Katika vifaa hivyo kwa Halmashauri ya Chalinze pekee tumeleta vyenye thamani ya sh. Mil. 236.6 ambapo hapa Msoga vimepata vya sh. Mil. 48.4," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Naye mganga mkuu wa chalinze Rahm Hangai alisema kuwa wameipongeza taasisi hiyo kwa msaada wao wa vifaa mbalimbali katika halmashauri ya chalinze kwenye idara ya afya.

Aidha amewataka wanachalinze kuwai kwenye vituo vya afya au hospital pindi wanapojihisi vibaya ili kuwai kupata matibabu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hiloRidhiwani Kikwete  akizungumza kwa niaba ya wananchi wake alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za kiafya kwa haraka na ukaribu zaidi .

Aliongeza kuwa vifaa hivyo vimefika kwa wakati mwafaka kutokana na kuwa hapo awali walikuwa na changamoto ya baadhi ya vifaa katika hospital hiyo lakini kwa msaada huu matatizo hayo yamepungua kwa asilimia kubwa na hivyo jamii sasa inapaswa kuvilinda vitu hivyo ili kusaidia vizazi na vizazi.
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete  na mkurugenzi wa taasisi ya THPS Syst Joseph wakikata utepe kukabidhi vifaa vyenye thamani ya sh. Mil. 48.4 kwa ajili ya kusaidia baadhi ya mahitaji ya kituo cha afya cha Msoga. 
 Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete  akimsalimia mtoto aliyefika katika  Kituo cha afya cha Msoga kwa ajili ya matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad