HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 13 August 2018

IGP AMPANDISHA CHEO MWANARIADHA KWA KUVUNJA REKODI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimpongeza Mwanariadha wa Polisi Fabian Nelson baada ya kumpandisha cheo kutoka Kostebo mpaka Koplo kutokana na kufanya vizuri katika Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanamichezo wote kwa kuchukua nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

Na. Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amempandisha Cheo Mwanariadha wa Polisi Fabian Nelson kutoka Konstebo hadi Koplo baada ya kuchukua medali ya dhahabu na kuvunja rekodi ya mbio za mita 5000 katika Michezo ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Mwanariadha huyo alikimbia dakika 13: 45: 99 na kuwashinda Wanariadha wa Jeshi la Polisi la Kenya na Uganda ambapo Tanzania ilishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza ilienda Kenya na ya tatu Uganda.

IGP Sirro alimpandisha Cheo hicho katika hafla ya kuwapongeza Wanamichezo walioshiriki Michezo hiyo katika bwalo la Maafisa wa Polisi Oystabya IGP Sirro alisema mwanariadha huyo amekuwa akionyesha juhudi katika mbio ndefu jambo ambalo limekuwa likileta sifa kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa Ujumla.

“ KIla mmoja anastahili pongezi kutokana na kutuwakilisha vizuri katika michezo hii, hivyo tunathamini mchango wa kila mmoja kwa nafasi yake katika kuitangaza nchi yetu na nawaahidi tutaendelea kutambua mchango wa kila mmoja” Alisema Sirro

Aidha, Alisema maandalizi ya michezo ijayo yanaanza sasa ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kufanya vizuri zaidi na kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika michezo ya mwaka huu ikiwemo kuingia kambini mapema na kuajiri wanamichezo pindi nafasi zitakapopatikana.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa alisema kazi iliyofanyika ni kubwa na kila mshiriki alijituma kuhakikisha kuwa Vikombe na medali zinabaki hapa nchini.

Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi, Taekwondo, Judo na Riadha ambapo nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, Sudani Kusini na Tanzania.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad