HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 23 August 2018

Hati za Kimila za Kumiliki Ardhi Kuwakomboa Wananchi Kiuchumi

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisisitiza kuhusu wananchi kutumia hati  za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha wakati wa hafla ya kuwakabidhi wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa hati hizo zilizotolewa baada ya maeneo yao kurasimishwa kwa kupimwa .
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akisisitiza umuhimu wa hati za kimila za kumiliki ardhi katika kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi wakati wa hafla ya kutolewa kwa hati hizo kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani kilosa ambapo Mpango huo kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya hiyo wamefanikisha upimaji wa ardhi katika Vijiji 37.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Magubike hati kimila ya kumiliki ardhi .
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisalimiana na viongozi wa Kijiji cha Magubike kabla ya kuanza kwa hafla ya kutoa hati za kimila kwa wananchi wa Kijiji hicho.
Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka MKURABITA  Bw. Japhet Werema akisisitiza umuhimu wa mpango wa kurasimisha ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa wakati wa hafla ya kutoa hati za kimila za kumiliki ardhi kwa wananchi wa Kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi walipata hati za kimila katika Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa pamoja na Watendaji wa Halmashuri na  wale wa  MKURABITA.
Mratibu wa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akifurahia ngoma za asili pamoja na kikundi cha ngoma hizo katika Kijiji cha Magubike  Wilayani Kilosa wakati wa hafla ya kukabidhi hati kwa wananchi wa Kijiji hicho.
Kikundi cha ngoma za asili cha Kijiji cha Magubike kikionesha umahiri wake katika kucheza ngoma hizo wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila za kumiliki ardhi kwa wananchi wa Kijiji hicho.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia hafla hiyo ya kutolewa kwa hati za kimila za kumiliki ardhi katika Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa.
Mratibu wa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akiwasikiliza baadhi ya wananchi mara baada ya hafla ya kutoa hati za kimila za kumiliki ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Magubike- Kilosa)

Frank Mvungi- MAELEZO, Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Bw. Adam Mgoyi  amewata wananchi kutumia fursa zinazotokana na urasimishaji ardhi uliowezesha kutolewa kwa hati zaidi ya 300 za kimila za kumiliki ardhi kwa wakazi wa Kata ya Magubike Wilayani humo jana.
Akizungumza na mamia ya wananchi  wa Kijiji hicho waliojitokeza katika hafla ya kutolewa kwa hati hizo amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano  ni kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wake kupitia mpango wa matumizi bora ya adhi  uliotekelezwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara  za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA)  na Halmashuri ya Wilaya hiyo.
“Tumieni hati hizi kutatua changamoto za kiuchumi kwani zinawawezesha kupata mitaji kutoka  katika taasisi za fedha  zilizopo ambazo zimeonesha nia yakuwawezesha wananchi na nyingine zimeanza kutoa mikopo kwa wananchi wetu wenye hati za kimila” Alisisitiza Mgoyi.
Akifafanua amesema kuwa hati  hizo zitasaidia kuondoa migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi na kuwapa wananchi uwezo wa kujiendeleza kiuchumi ambapo tangu MKURABITA ianze zoezi la urasimishaji ardhi Wilayani humo wananchi wengi wamenufaika na mikopo iliyowawezesha kuwa na kilimo chenya tija.
Aliongeza kuwa Vijiji 37 vimenufaika na mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Wilaya ya Kilosa ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“ Halmashuri ya Wilaya inao wajibu wa kutenga sehemu ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wananchi katika upimaji wa ardhi na kuleta mpango bora wa matumizi ya Ardhi” Alisisitiza Mgoyi.
Pia kwa kuzingatia umuhimu wa kurasimisha ardhi Mgoya alibainisha kuwa mpango huo  unasaidia kubainisha maeneo ya ufugaji na yale ya kilimo katika Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mratibu wa MKURABITA Bi. Serapia Mgembe amesema kuwa wananchi wa  Wilaya hiyo ambao maeneo yao yamerasimishwa na kupimwa watumie fursa hiyo kushiriki katika kujiletea maendeleo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Aliongeza kuwa Serikali inafanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora hivyo jukumu lao ni kuunga mkono kwa kutumia fursa zinazoletwa na Serikali kupitia mpango wa matumizi bora ya Ardhi uliwawezesha kupimwa na hatimaye kuwapatia hati za kimila za kumiliki maeneo hayo.
Mpango wa Kurasimisha Biashara  na Rasilimali za Wanyonge Tanzania umetajwa kuwa chachu ya mageuzi ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa na hivyo kuleta ustawi wa wananchi kiuchumi baada ya kupata hati za kimila za kumiliki maeneo yao yakiwemo mashamba na Viwanja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad