Frank Mvungi- MAELEZO, Lindi
Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na
Idara ya Habari (MAELEZO) wameanzisha utaratibu wa kufuatilia utendaji wa maafisa
habari katika ngazi zote na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha
mawasiliano kati ya Serikali na Wananchi.
Akizungumza Mjini Lindi Kiongozi wa Ujumbe kutoka TAGCO na Idara ya Habari
MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa dhamira ya ziaraa katika
Halmashuri ya Manispaa hiyo na maeneo mengine hapa nchini ni kuona changamoto
zinazowakabili maafisa Habari katika kutekeleza jukumu la kuisemea Serikali na
kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia katika kutatua changamoto zilizopo.
“ Ziara yetu inalenga kuona namna maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la
kuisemea Serikali katika Manispaa ya Lindi hasa kutangaza miradi inayotekelezwa na
Serikali kwa manufaa ya wananchi” Alisisitiza Simwanza
Akifafanua Bi. Simwanza amesema kuwa Halmashuri zinalo jukumu la kuwawezesha
maafisa hao ili waweze kutekeleza jukumu la kuisemnea Serikali katika maeneo yao
hasa kutoa taarifa za miradi inayotekelezwa akitolea mfano wa ujenzi wa barabara za
Lami katika Manispaa hiyo ambao umefanyika kwa kiwango kikubwa na kubadili
taswira ya mji huo na kuwa ya kuvutia.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya Lindi Bw. Babtista
Kihanza amesema kuwa Ofisi yake iko tayari kuweka mazingira wezeshi kulingana na
upatikanaji wa rasilimali ili kuwezesha mawasiliano kati ya wananchi na Serikali
kuimarika hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo.
“ Sisi tuko tayari kumuwezesha afisa habari wetu kadiri rasilimali zitakavyoruhusu ili
aweze kufanikisha jukumu la kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na
Serikali.” Alisisitiza Babtista
Kwa upande wake mwakilishi wa Idara ya Habari MALEZO Bw. Casmir Ndambalilo
amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanapata taarifa za miradi ya
maendeleo kwa wakati muafaka ili waweze kutumia fursa za miradi hiyo kujiletea
maendeleo.
Aliongeza kuwa ni vyema maafisa habari katika Mikoa na Halmashauri wakatumia
mbinu za kisasa katika kuwasiliana na wananchi katika maeneo yao kwa kutoa taarifa
za miradi yote inayoteklezwa na ile inayotarajiwa kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment