HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 23, 2018

Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi

Na mwandishi wetu
VETERANI wa timu ya soka ya Uingereza ya Liverpool, Sami Hyypia amewataka vijana Watanzania kuongeza bidii katika kuhakikisha kwamba wanafikia hatua za juu za uchezaji soka hivyo kupata nafasi ya kucheza Ulaya.
Pia amesema ni matumaini yake kuwa mamlaka za utoaji leseni hazitawazuia vijana kwenda Ulaya kujaribu bahati zao.
Alisema hayo wakati wa kiliniki ya soka aliyoifanya kwa vijana wa Serengeti boys jana alipokuwa akishiriki nao katika mafunzo na mazoezi.
Alisema kwamba yeye hakuwa na kipaji kikubwa kuliko alivyoviona kwa vijana hao lakini ameweza kufikia hatua za juu kabisa za uchezaji wa soka kutokana na kujituma kwake.
Alisema amewaambia vijana kuangalia zaidi juhudi kwani kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu kuwa gwiji katika soko.
Alisema pamoja na mafundisho ya walimu ni kazi ya mchezaji mwenyewe kuona udhaifu wake uliopo na kuufanyia kazi ili aweze kuwa mwanasoka bora wa kutegemewa.
Akihojiwa mwanasoka huyo ambaye aliwika sana katika enzi zake alisema kwamba amefurahishwa na uchezaji wa timu hiyo hasa kwa pasi ndefu na kusema kwamba vijana wote wameonesha kuwa na vipaji vikubwa.
Alisema hata hivyo kwamba amewaambia wachezaji awali kuwa na kipaji pekee hakutoshi lakini ni lazima mtu binafsi kufanyakazi ya ziada kuondoa udhaifu wake ambao binadamu wengi wanakuwa nao ili kuwa mahiri katika uchezaji.
Sami ambaye yupo nchini kuangalia michuano ya kombe la benki ya Standard Charted  inayofanyika leo na kushirikisha timu 32 zinazowania kwenda Anfield kuona mechi za msimu mpya timu ya Liverpool  ndani ya EPL na kuzungumza na magwiji na kupata nafasi ya kunolewa, amesema siri kubwa ya mafanikio ni kujituma kwa mchezaji pamoja na kwamba anakipaji na walimu wazuri.
Naye  Oscar Milambo mkufunzi wa timu ya vijana alisema kwamba amefurahishwa sana na kuja kwa gwiji huyo nchini na kushiriki katiika kliniki ya soka.
Alisema pamoja na mafundisho, kuwapo kwa Sami kumesaidia kuwajenga vijana kisaikolojia hasa kuhusiana na suala la kujituma.
Alisema anaamini kwamba vijana wamesikia na kuzingatia maelezo ya gwiji huyo ambaye aliwataka vijana kujituma pamoja na kwamba wapo na vipaji ili kuweza kufikia hatua za juu za uchezaji soka.
Alisema gwiji huyo amewapa faraja kubwa kwa kuja na kwamba wanaendelea na maandalizi ya kwenda Algeria kama sehemu ya kuendelea kujiandaa na michuano mbalimbali kabla ya Afcon 2020.
Wakati huo huo Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba amesema kwamba benki yake inafuraha kuendelea kusaidia kukuza vipaji vya vijana nchini kwa kutumia magwiji wa Liverpool.
Alisema benki yake ni wadhamini wa timu hiyo na wamekuwa wakihakikisha kwamba wanashirikiana kukuza vipaji katika nchi ambazo benki inafanyabiashara zake.
Alisema mwaka jana walimleta John Barnes ambaye pia aliendesha kliniki ya soka hali ambayo inaimarisha utaalamu na kisaikoilojia kwa vijana.
Alisema ni lengo la benki hiyo kuhakikisha kwamba wanawaleta wataalamu kuboresha vipaji vya soka kukua nchini.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akimtambulisha Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) kwa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kulia) pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza kwa makini Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) na Mshauri Mkuu wa Ufundi katika Programu za Soka la Vijana nchini, Kim Paulsen wakiangalia uzoefu wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.


 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.
 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakijinoa baada ya kupata mafunzo na mbinu mbalimbali wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia hapa nchini.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kliniki ya soka kwa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha kliniki ya soka kwa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliishukuru benki ya Standard Chartered kwa kudhamini ujio wa Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia  (hayupo pichani) na kuendesha kliniki ya soka kwa vijana wake iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akipeana mikono na kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) mara baada ya kliniki ya soka kumalizika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. 
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia katika picha ya pamoja na kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) sambamba na uongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo mara baada ya kliniki ya soka kumalizika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad