HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 June 2018

HUKUMU KESI YA WEMA SEPETU MATUMIZI DAWA ZA KULEVYA KUTOLEWA JULAI 16

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 16 mwaka 2018 inatarajia kusoma hukumu ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii maaruifu wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Sepetu na wafanyakazi wake wawili.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa upande wa utetezi, Albert Msando kuwasilisha hoja za majumuisho katika kesi hiyo za kushawishi Mahakama iwaone wateja wake hawana hatia.

Wakati Wakili wa upande wa mashtaka Costantine Kakula akiwasilisha hoja za majumuisho ili Mahakama iwaone washtakiwa wana hatia.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wema na wafanyakazi wake kumaliza kujitetea na upande huo wa utetezi kufunga kesi yao.

Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Akijitetea katika kesi hiyo, Wema alikubali kuwa nyumbani kwake palikutwa na msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi jikoni na katika chumba cha kuhifadhia nguo zake.Pia walikuta kiberiti katika chumba wanacholala wanamuziki hao wawili Jodarn na Mila.

Akiongozwa na Wakili Msando alidai Februari 3 mwaka 2017 alitakiwa kuripoti polisi kwa tamko la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Ambapo akiwa na watu wengine, walifika pale saa tano asubuhi na kusubiri hadi saa 10 jioni, ambapo Makonda alifika na kuwaita mmoja mmoja katika chumba ambacho alikuwepo na Afande Sirro" Ameeleza Wema.
Amedai moja kati ya maswali waliyomuuliza ni kama alikuwa akitumia au kuuza dawa za kulevya lakini aliwajibu hapana.

Aliendelea kudai kuwa baada ya mahojiano hayo walipelekwa mahabusu ambapo walikaa kwa siku saba na kati ya siku hizo, Februari 5 mwaka 2017 Jumapili polisi, akiwamo afande Mery,OCID Denis, Hassani walimpeleka kwake kufanya upekuzi.

Alidai hajui hizo bangi ni za nani ingawa polisi walizikuta nyumbani kwake, kwa sababu yeye kwa asili ya kazi yake ya usanii nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya pati mara kwa mara na kualika marafiki zake.

“Nyumba yangu inaingia watu wengi tofauti tofauti, siwezi kujua hivyo, vitu viliingizwa na kina nani maana kila anayefika kwangu anauhuru wa kuingia katika chumba chochote kasoro chumbani kwangu tu,”ameeleza Wema

Ameongeza kuwa, muda wote walipokuwa njiani kwenda kwa kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake hawakuzungumza chochote na afande Mery.

Bali baada ya kurudishwa kituoni alichukuliwa sampuli ya mkojo pale pale Polisi na kwamba alimkabidhi afande Mery.

Wakijitetea wafanyakazi wa Wema, Angelinana Matrida wao walieleza kuwa wakati askari walipoenda kufanza upekuzi kwa Wema wao walikuwa wamekaa nje.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februar 4 mwaka 2017 huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi mwaka 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Bangi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad