HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 28 June 2018

Halotel, StarTimes waleta kombe la dunia kiganjani

Bando hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana.

Huku mshike mshike wa kombe la dunia ukiendelea kukolea, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel kwa kushirikiana na Kampuni ya StarTimes wameleta wamezindua huduma mpya itakayo wawezesha wateja wa mtandao huo kuangalia mechi za kombe la dunia kupitia simu zao za kiganjani kwa gharama nafuu.

Huduma hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana, huduma hiyo inawapatia wateja intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda amesema huduma hiyo itawawezesha wateja wa Halotel nchini nzima kufurahia kutazama mechi za kombe la dunia kupitia simu za mikononi (Smartphone) kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwa kutumia intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.

“Kuanzia sasa wateja wa Halotel wanaweza kupakua Application ya Startimes kupitia simu zao za Android na watalipia kuanzia shilingi 2000 na watapata GB 1 ambayo wanaweza kuitumia kuangalia mechi zote za kombe la dunia kwa intaneti yenye kasi. Alisema Semwenda.“Jinsi ya kufanya malipo mteja wa Halotel anapaswa kufungua Application ya Star times na baada ya hapo atafuata maelekezo ya kununua vifurushi kuanzia vya siku, wiki hadi mwezi mzima,” Alihitimisha Semwenda.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa StarTimes Ndg. David Malisa Alisema, “Ukiwa unatumia intaneti ya Halotel ni rahisi zaidi kulipia na kutumia StarTimes App ambayo ina burudani na mechi zote za Kombe la Dunia. Kwa watumiaji wa mitandao mingine wanalipia maudhui pembeni na intaneti au data pembeni, ukilipia huduma hii unakuwa umelipia maudhui na intaneti kwa pamoja. Pia unaweza kutumia Intaneti hii bila kikomo kwa masaa 24 hata bando inapoisha utaendelea kupata Intaneti ya kutumia kwenye StarTimes App”. Alisema Malisa. 

Hii ni huduma ya kwanza kabisa Tanzania ambayo itamruhusu mteja kuendelea kupata intanenti hata baada ya bando lake kuwa limekwisha. Ushirikiano baina ya StarTimes na Halotel ni katika hatua ya kusogeza Burudani ya kandanda la kimataifa katika Simu za Mkononi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel (kulia) akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kushoto ni Meneja Masoko wa Startimes David Malisa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa kwa pamoja wakionesha namna ambavyo mteja wa Halotel anavyoweza kuangalia mpira kwenye simu yake ya mkononi kupitia App ya Star times. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa pamoja katika uzinduzi wa Halotel na Startimes kuonyesha ishara ya ushirikiano.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad