HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 14, 2018

WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO

Wataalam kutoka  Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamefanya  ziara katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni vilivyopo mkoani Morogoro. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa, kampuni ya State Grid iliyopewa kazi hiyo katika mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwasha umeme katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni tarehe 16 Mei, 2018.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ziara hiyo. Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Yusuph Msembele.
 Moja ya transfoma zilizofungwa na kampuni ya State Grid katika kijiji cha Mandera   kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO- Kanda ya Kati, Mhandisi Atanasius Nangali ( wa pili kulia) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (kushoto) akimsikiliza  mwananchi wa kijiji cha Kibaoni kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Joseph Mkude (kulia) katika ziara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad